Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aga Khan: Wanaojua kusoma, kuandika wameongezeka

Mkurugenzi Mkuu  wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Afrika Mashariki ya Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU-IED EA),Profesa Joe Lugalla (wa kwanza kulia ) pamoja na  wahadhiri wa taasisi hiyo wakiangalia vitabu jana jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kujua kusoma. Picha na Mpiga Picha wetu.

Muktasari:

  • Changamoto hiyo ipo kwa rika zote watoto na watu wazima wa vijijini na mijini, huku takwimu za dunia zikionyesha watu wazima milioni 750 na watoto 264 milioni wamekosa elimu ya msingi ya kujua kusoma na kuandika.

Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Afrika Mashariki ya Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU-IED EA), imesema kiwango cha watu kujua kusoma na kuandika Tanzania kimekuwa kikiongezeka licha ya uwapo wa baadhi ya changamoto.

Changamoto hiyo ipo kwa rika zote watoto na watu wazima wa vijijini na mijini, huku takwimu za dunia zikionyesha watu wazima milioni 750 na watoto 264 milioni wamekosa elimu ya msingi ya kujua kusoma na kuandika.

Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Joe Lugalla alisema hayo jana wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wanaojua kusoma na kuandika. AKU-IED EA iliungana na wadau mbalimbali kuadhimisha siku hiyo.

Profesa Lugalla alisema teknolojia ya kidigitali imebadilisha mambo mbalimbali, ikiwamo elimu na utendaji wa kazi na maisha na kwamba inatoa fursa katika upatikanaji wa taarifa, huduma za jamii na viwanda.

“Teknolojia ya kidigitali inatoa fursa hizi lakini watu hawawezi kunufaika nazo, iwapo hawatakuwa na msingi wa kujua kusoma na kuandika,” alisema Profesa Lugalla.

Alisema ili nchi iendelee lazima iwe na watu wenye afya na elimu bora itakayosaidia fursa ya kujenga mazingira na kuliendeleza Taifa.

Profesa Lugalla alisema Septemba 8 imetengwa duniani kuenzi umuhimu wa watu kujua kusoma, kuandika na kuhesabu na kwamba ni muhimu katika kujenga uelewa na ujuzi utakaoleta maendeleo ya nchi husika.

Naye Mhadhiri Msaidizi wa taasisi hiyo, Profesa Mary Oluga alisema kuna changamoto kwa shule za awali na sekondari kuhusu kusoma hasa kutokana na kutokuwa na vifaa vya kutosha, walimu na ufundishaji.