Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi, wafuasi Chadema wajitokeza mahakamani kufuatilia uamuzi kesi ya Lissu

Muktasari:

 Viongozi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamejitokeza katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam kufuatilia kesi ya Tundu Lissu.

Dar es Salaam.  Viongozi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamejitokeza katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam kufuatilia kesi ya Tundu Lissu.


Lissu amefungua shauri la maombi mahakamani hapo akipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu kuahirisha usikilizwaji wa kesi ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni, uliotolewa Juni 2, 2025.


Uamuzi huo unatarajia kutolewa leo Ijumaa Julai 11, 2025 na  Jaji Elizabeth Mkwizu anayesikiliza shauri hilo, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili yaani mawakili wa Serikali na mawakili wa Lissu.

Tayari Jaji Mkwizi ameshaingia katika Mahakama ya wazi namba moja kwa ajili ya kusoma uamuzi.


Tofauti na siku nyingine, leo Lissu alivyopandishwa kizimbani katika Mahakama ya wazi, alikuwa mtulivu na kusalimia mawakili wake na wafuasi wake kwa sauti ya kawaida, tofauti na siku nyingine ambapo hupaza sauti na kuonyesha ishara ya vidole viwili juu.


Hata hivyo, ulinzi umeimarishwa ambapo askari kadhaa wenye sare na wasiokuwa na sare za jeshi hilo wametawanywa kuanzia nje ya geni mpka ndani ya mahakama.

Endelea kufuatilia mwananchi