Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajali ya basi, daladala yaua wawili akiwemo mwenyekiti UWT


Muktasari:

  • Majeruhi wa ajali hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga

Tabora. Watu wawili akiweno Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora, Zawadi Angelo maarufu Mama Sukuma wamefariki dunia katika ajali ya basin a daladala.

Ajali hiyo imetokea saa 9:30 alasiri ya leo Ijumaa, Julai 19, 2024 katika Kijiji cha Nanga, Wilaya ya Igunga ikihusisha basi la Mumuki lililokuwa likitoka mkoani Katavi kwenda Mkoa wa Arusha lililogongana uso kwa uso na gari dogo la abiria maarufu daladala.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema majeruhi watano wa ajali hiyo wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga. Jina la marehemu mwingine halijafahamika.

Kamanda Abwao amesema dereva wa basi la Mumuki anashikilia kwa mahojiano zaidi ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa hatua akidai hakuchukua tahadhari wakati akiendesha chombo cha moto.

"Chanzo cha ajali na namba za usajili wa magari bado tunachunguza na taarifa ikikamilika tutawapatia, lakini niendelee kutoa wito kwa madereva wa mabasi ya masafa marefu kuendelea kuchukua tahadhari za usalama barabarani kwa lengo la kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara," amesema.

Naye Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Igunga, Peter Kalindo amesema wamepokea kwa masikitiko kifo cha mwenyekiti wao.

"Sisi kama chama tumepokwa kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwenyekiti wetu wa Umoja wa wanawake Wilaya ya Igunga," amesema Kalindo na kuongeza;

"Baada ya taarifa za kifo chake tunawasiliana na familia yake ili kupata ratiba kamili ya mazishi yake hivyo tunawaomba watu wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu kwetu."


Endelea kufuatilia Mwananchi.