13 wafariki dunia ajali ya basi la Ally's kugonga treni

Singida. Watu 13 wamefariki dunia huku 32 wakijeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Ally's Star lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga treni ya mizigo katika makutano ya barabara na reli maeneo ya Manyoni Mkoa wa Singida.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Novemba 29, 2023, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni, Dk Furaha Mwakafilwa amesema wamepokea mili ya watu 13 na majeruhi 32.
Taarifa zinaeleza, ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Jumatano.
Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa taarifa zaidi