Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simulizi ya mkazi wa Mbeya aliyepata ajali Mtwara

Baadhi ya mabalozi wa Usalama barabarani (RSA)  pamoja na askati wa usalama baranarani wa Mkoa wa Mtwara wakimjulia hali mhanga wa ajali ya barabarani  Cosmas Maravugi mkazi wa mkoani Mbeya  katika maadhimiaho ya wahanga wa ajali za barabarani. Picha na Florence Sanawa

Mtwara. Mmoja wa majeruhi wa ajali za barabarani, Cosmas Maravugi ambaye ni mkazi wa mbeya amejikuta akiingia katika maumivu makali baada ya kupata ajali akiwa kazini kama kondakta wa gari kubwa la mizigo mkoani Mtwara.

Akizungumza wodini katika Hospitlai ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, baada ya kutembelewa na mabalozi wa Usalama barabarani (RSA) leo Jumapili Novemba 19, 2023, Maravugi amesema kuwa amepata ajali baada ya kufika Mtwara akitokea mkoani Mbeya ambapo alikuwa kondakta wa gari ambayo ilipeleka bidhaa soko kuu Mtwara.

Amesema kuwa baada ya kufika sokoni alishuka ili kuangalia sehemu itakayofaa kwaajili ya kushusha mzigo waliokuwa wanauleta sokoni.

“Kwa hali niliyonayo kwa sasa inatia matumani  yaani nimegongwa na gari yangu mwenyewe nilikuwa kama utingo nikitokea Njombe nikaingia sokoni mtwara na gari yangu ndio ilinikanyaga nilipiga kelele sana dereva alisikia akasimamisha gari.

“Yaani tulitoka safari ndefu sana lakini nilishuka ili niondoe bidhaa zilizokuwa zimezuia geti la kuingilia sokoni ambapo nilipokuwa nazitoa shati langu likanasa kwenye kapu la uchafu wakati najaribukutoa gari ikarudi nyuma ghafla ndio ikanikanyaga na kunisababishia maumivu makali” amesimulia Cosmas.

Naye Muuguzi Kiongozi wa Hosptali ya Rufaa ya mkoa wa Mtwara  Ligula,  Hawa Mamanga amesema kumekuwa na majeruhi wengi wa ajali za barabarani ambao wanafikishwa hospitalini hapo.

“Hapa tunapokea ajali nyingi za barabarani ingawa tunapokea pia ajali za  kuungua moto na wengine kugongwa na nyoka  lakini  wanaopata ajali za bodaboda  ni wengi zaidi” amesema Namanga

Mwakilishi wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mtwara, Sada Mkudili  amesema kuwa ikiwa ni siku ya wahanga wa ajali za barabarani duniani mkoa wa mtwara umeadhimisha kwa kautembelea wagonjwa hospitalini waliopata ajali mbalimbali  na kuwajulia hali sambamba na kuwatembelea kituo cha kulelea watoto yatima.

“Ajali za barabarani zimekuwa ni changamoto ya dunia nzima ambapo zaiid ya watu milioni1 hufa ambapo waathirika zaidi ni watoto hili kwetu ni tishio kwetu na dunia kwa ujumla” amesema Mkudili

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Bahati Mwakasambala amesema kuwa wameungana na mabalozi ili kuadhimisha siku hii ya wahanga watokanao na ajali nchini.

“Ajali zipo kwa kutambua kuwa hilo tumekuwa tukitoa elimu endelevu ili kuweza kuepukana na hili janga la ajali ambapo tunapita kwenye shule za sekondari na msingi, vijiwe vya bodaboda na bajaji lazima tutambue kuwa yeyote anayetumia barabara anaweza kupata ajali, haina mwenyewe wala haina muda ndio maana tunasisitiza na kutoa elimu za mara kwa mara,” amesema Mwakasambala