Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili wahofiwa kufariki dunia ajalini Tabata

Muktasari:

  • Watu wawili wanadaiwa kufariki dunia kutokana na ajali iliyohusisha Lori na pikipiki.

Dar es Salaam. Watu wawili wanadaiwa kupoteza maisha kutokana na ajali ya pikipiki iliyogongana na lori jijini hapa.

Ajali hiyo imetokea eneo la Tabata Gereji jijini Dar es Salaam na kulingana na mashuhuda wa tukio hilo, wanaodaiwa kupoteza maisha ni dereva wa pikipiki na abiria wake.

Mwananchi Digital leo, Novemba 12, 2023 imefika katika eneo la tukio na kushuhudia miili ya watu wawili ikisafirishwa na gari la kubebea wagonjwa.

Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa mashuhuda Patrick Duma amesema ajali imesababishwa na lori kuhama njia.

Amesema lori hilo lilihama njia lilipojaribu kulikwepa lingine lililosimama barabarani kwa matengenezo.

"Dereva naona breki zilifeli akashindwa kwenda kuligonga lile Lori bovu akaamua kuhama njia ndiyo amekutana na bodaboda na kumgonga," amesema.

Amesema si bodaboda wala abiria aliyepona katika tukio hilo, kwani miili yao imeharibiwa.

Kulingana na Patrick, Lori hilo lilikuwa linatokea Ubungo kufuata uelekeo wa Buguruni, huku pikipiki ikitokea Buguruni kuelekea Ubungo.

Hata hivyo, amesema baada ya ajali hiyo dereva wa Lori amekimbilia kusikojulikana.

Shuhuda mwingine, amesema hatua ya lori lililoharibika kuachwa kwa takriban siku mbili bila kuondolewa barabarani ndiyo sababu ya ajali hiyo.

"Haiwezekani Lori lile limeharibika kwa karibu siku mbili bado lipo barabarani, lilipaswa kutolewa, dereva walLori lililopaswa ajali alikuwa anajaribu kulikwepa lile bovu," amesema.

Hadi Mwananchi digital inaondoka katika eneo la tukio, bado hayakutambulika majina ya wanaodaiwa kupoteza maisha, huku juhudi za kuliondoa Lori hilo na pikipiki zilizotumbukia mtaroni zilikuwa zikiendelea.