Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu Kweka afariki dunia

Askofu Mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Erasto Kweka enzi za uhai wake.

Muktasari:

  • Dk Erasto Kweka amekuwa kiongozi wa Dayosisi ya Kaskazini tangu mwaka 1976 mpaka 2004 alipostaafu.

Moshi. Askofu Mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Erasto Kweka amefariki dunia leo Novemba 25, 2023, kweye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), alilokuwa anapatiwa matibabu.

Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa hilo, Zebadiah Moshi kupitia taarifa yake aliyoitoa leo, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa, Dk Kweka amekuwa kiongozi wa Dayosisi ya Kaskazini toka mwaka 1976 mpaka 2004 alipostaafu.

“Uongozi wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini una masikitiko makubwa kutangaza kutwaliwa kwa baba Askofu Mstaafu Dk Erasto Kweka, kifo kimetokea leo, Novemba 25, 2023 saa nne asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa “Uongozi wa dayosisi utaendelea kuwajulisha mipango ya mazishi, pale itakapokamilika, nawatakia baraka za Mungu,”