Askofu Mwenisongole afariki dunia

Muktasari:
- Askofu Mkuu mstaafu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk Ranwell Mwenisongole amefariki dunia jana Jumamosi Desemba 25, 2021 katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Morogoro. Askofu Mkuu mstaafu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Dk Ranwell Mwenisongole amefariki dunia jana Jumamosi Desemba 25, 2021 katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Mwenisongole amefariki akiwa na umri wa miaka 75.
Akizungumza na Mwananchi Digital, Askofu mkuu wa kanisa hilo, Dk Barnabas Mtokambali amesema Dk Mwenisongole amefariki wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Lugalo.
Imeelezwa kuwa sababu ya kifo cha Askofu Mwenisongole ni mshtuko wa moyo.
Maziko yatafanyika katika jimbo la kanisa TAG Songwe Mashariki Vwawa wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe Desemba 30 mwaka huu.
“Baada ya kustaafu uaskofu mkuu kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk, Ranwell Mwenisongole alikuwa Mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG City Christian Centre (CCC) Upanga Dar es Salaam jimbo la Mashariki kati kusini hadi umauti ulipomkuta.”amesema Dk Mtokambali.