Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanajeshi Niger wadai kumtoa Rais madarakani

Niger. Wanajeshi nchini Niger Jana Jumatano Julai 27, 2023 wametangaza kumtoa madarakani Rais wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum kwa madai ya kushindwa kutawala vizuri na kushindwa kusimamia usalama.

Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Niger, Kanali Amodou Abramane katika kituo cha Taifa cha Runinga nchini humo cha West Africa TV.

"Tunautamatisha utawala huu, Kama mnavyojua kwasababu ya kushindwa kuwa na utawala bora na kushindwa kusimamia vizuri usalama wa nchi," amesema Kanali Abramane akiwa amezungukwa na wanajeshi wengine.

Aidha, Abdramane amesema mipaka ya Niger imefungwa, amri ya kutotoka nje imetangazwa nchini kote, na taasisi zote za jamuhuri zimesitishwa.

Wanajeshi hao walionya dhidi ya uingiliaji kati wowote wa mataifa ya kigeni katika mapinduzi hayo.

Kuchukuliwa kwa jeshi kwa nchi hiyo yanafanya idadi ya mapinduzi kufikia saba katika eneo la Afrika Magharibi tangu mwaka 2020 jambo linalotajwa huenda likasababisha ugumu wa kupambana na ugaidi katika maeneo hayo.

Rais Bazoum aliingia madarakani kwa kufanyika uchaguzi wa kwanza wa mpito kidemokrasia katika jimbo ambalo limeshuhudia mapinduzi manne ya kijeshi tangu uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960.