Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trump asitisha misaada ya maendeleo nje ya Marekani

Muktasari:

  • Hii ni mara ya pili kwa Trump kupendekeza kupunguza misaada ya kigeni, akilenga kutoa misaada kwa nchi zinazoheshimu Marekani.

Dar es Salaam. Rais wa Marekani, Donald Trump, amesitisha misaada ya maendeleo ya nje kwa siku 90, kupisha tathmini ya ufanisi na uwiano na sera yake ya kigeni.

Agizo hilo amelolitoa siku moja baada ya kuapishwa kwa muhula wake wa pili, limeelezwa kuwa ni amri ya kiutendaji, iliyosainiwa na rais huyo.

"Viongozi wote wa idara na mashirika yenye jukumu la mipango ya misaada ya maendeleo ya nje ya Marekani, wanapaswa mara moja kusitisha majukumu mapya na matumizi ya fedha za misaada ya maendeleo," imeeleza amri hiyo.

Haikuwa wazi mara moja ni kwa upana gani agizo hilo lililenga na ni mipango gani, nchi, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kimataifa yanayohusika na hatua hiyo.

Pia haikufahamika fedha gani zinaweza kukatwa, ikizingatiwa kuwa Bunge la Marekani ndilo huweka bajeti ya Serikali ya shirikisho la Marekani.

Amri hiyo ya kiutendaji inarudia mtazamo aliokuwa nao Trump wakati wa muhula wake wa kwanza kati ya mwaka 2017 na 2021.

Alipoingia madarakani, alipendekeza kupunguza takriban theluthi moja ya bajeti za diplomasia na misaada ya Marekani, ikiwa ni pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa ufadhili wa shughuli za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa.

Hata hivyo, Bunge la wakati huo lilipinga mapendekezo ya Trump.

Kisha, kwenye mkusanyiko wa kila mwaka wa viongozi wa dunia katika Umoja wa Mataifa mwaka 2018, Trump alilalamika kwamba Marekani ilikuwa mfadhili mkubwa wa misaada ya kigeni, lakini ni wachache tu ndio wanawapa chochote.

"Ndiyo maana tunachukua mtazamo wa kina juu ya misaada ya nje ya Marekani.

"Tukiendelea mbele, tutatoa misaada ya nje kwa wale tu wanaotuheshimu na kwa kweli, ni marafiki wetu," alisema Rais Trump katika muhula wake wa kwanza.