Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tinubu wa chama tawala aongoza kwa kura Nigeria

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo

Muktasari:

  • Ikiwa ni siku mbili baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wenye mchuano mkali zaidi katika historia nchini Nigeria, chama tawala cha APC kinaongoza kwa kura nyingi katika matokeo ya awali.

Dar es Salaam. Mgombea urais wa chama cha All Progressives Congress (APC) nchini Nigeria, Bola Tinubu anaongoza kwa kura katika majimbo 20 kati ya 36 katika kinyang’anyiro cha urais, huku vyama vya upinzani vikijiondoa katika mchakato wa kuhesabu kwa madai ya udanyanyifu.

Kwa mujibu wa Reuters, matokeo ya tume ya muda ya uchaguzi yameonyesha Tinubu amekuwa mbele kwa asilimia 39.7 ya kura halali zilizohesabiwa, dhidi ya asilimia 32.2 ya kura za Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani cha People's Democratic Party (PDP).

Naye Peter Obi wa chama kidogo cha Labour akiwa katika nafasi ya tatu kwa takriban asilimia 16.3 ya kura.

Uchaguzi huo umekumbwa na changamoto ya vifaa na teknolojia ambayo yamesababisha kudorora kwa zoezi la majumuisho katika maeneo mengi katika kuweka matokeo moja kwa moja kutoka kila kituo cha kupigia kura kwenye tovuti.

Kushindwa kwa tume ya uchaguzi kutimiza ahadi yake ya uwazi kulisababisha matokeo yakusanywe kwa mikono ndani ya vituo vya kuhesabia kura vya kata na serikali za mitaa kama katika uchaguzi uliopita.

"Ukosefu wa INEC wa mipango madhubuti katika hatua muhimu na mawasiliano madhubuti ya umma yamepunguza imani katika mchakato huo," ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya umesema katika taarifa.


Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Jumuiya ya Madola ambaye pia ni Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki pia ameikosoa INEC kwa kushindwa kuweka matokeo kwenye tovuti.

Hadi kufikia saa 01:00 jioni jana Jumatatu, INEC ilikuwa imepakia matokeo kutoka kwenye vituo 66,167 tu kati ya 178,846, tovuti yake imeonyesha.

"Tunawajibika kikamilifu kwa matatizo hayo na tunajutia usumbufu ambao umetokea kwa wagombea, vyama vya siasa na wapiga kura," ilisema taarifa ya tume hiyo.

Vyama vya upinzani vilionyesha kutoridhika na matokeo hayo.

"Mchakato wa uchaguzi umeibiwa na tunajitenga nao kabisa," msimamizi wa kampeni wa PDP Atiku Melaye Dino amesema katika kituo cha matokeo cha INEC huko Abuja.

Naye Mkurugenzi wa kampeni wa Obi, Akin Oshintokun ameulalamikia uchaguzi huo akisema;

"Tunajuta kusema kwamba tumepoteza imani na matokeo yanayokusanywa na kutangazwa," amesema.