Obi wa upinzani ashinda jimbo la Lagos

Peter Obi
Lagos. Mgombea urais nchini Nigeria anayepewa nafasi ya tatu Peter Obi ameshinda Jimbo la Lagos, baada ya kumbwaga mgombea wa chama tawala mwenye ushawishi mkubwa Bola Tinubu, kulingana na matokeo yaliyotangazwa kutoka kituo cha kura cha jimbo hilo.
Ushindi wa Obi umeshangaza wengi kwani jimbo hilo ni ngome ya Tinubu, ambaye alitarajiwa kushinda jimbo hilo kwa urahisi.
Kwa mujibu wa CNN, Tinubu ni gavana wa zamani wa Jimbo la Lagos na anajulikana zaidi kutokana na ushawishi wake mkubwa kisiasa.
Obi mwenye miaka 61, amepata umaarufu miongoni mwa vijana hasa, wengi wanaojiita ‘Obidients’ yenye maana watii
Uchaguzi huo unatajwa wenye ushindani mkali zaidi nchini humo tangu 1999 huku vyama viwili ambavyo vimetawala siasa za Nigeria tangu wakati huo vikikabiliwa na tishio ambalo halijawahi kushuhudiwa kutika Chama cha Labour cha Obi.