Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Israel, Iran waendelea kupambana, Rais Donald Trump ataka amani

Yerusalem/Dubai. Machafuko kati ya Israel na Iran yameingia katika sura mpya ya umwagaji damu baada ya mataifa hayo mawili kuendeleza mashambulizi makali leo Jumapili na kuua watu wengi.

Wakati hayo yakijiri, Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa mgogoro huo unaweza kumalizwa kwa urahisi, huku akiitishia vikali Iran iwapo itashambulia mali au masilahi yoyote ya Marekani.

Katika miji mbalimbali ya Israel, vikosi vya uokoaji vinaonekana vikichimba vifusi vya majengo ya makazi yaliyoporomoka kutokana na mashambulizi ya makombora, wakitumia tochi na mbwa maalumu wanaonusa, wakitafuta manusura. Mamlaka zimeripoti kuwa watu wasiopungua 10 wamefariki dunia, wakiwamo watoto.

Iran imetangaza kuwa watu wasiopungua 138 wameuawa tangu Ijumaa kufuatia mashambulizi ya Israel, akiwamo mtoto mmoja kati ya kila wawili waliouawa Jumamosi, wakati kombora lilipoangusha jengo refu la ghorofa 14 katika mji mkuu wa nchi hiyo.

Jeshi la Israel limetoa onyo kwa wananchi wa Iran wanaoishi karibu na maeneo ya kijeshi au ya kuhifadhi silaha, kuondoka mara moja kwa usalama wao, huku Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, pamoja na Trump wakieleza kuwa mashambulizi hayo yataongezeka badala ya kupungua.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Mmoja wa maofisa wa kijeshi wa Israel amesema kuwa bado wana orodha ndefu ya maeneo ya kushambulia ndani ya Iran, na amekataa kueleza ni kwa muda gani mashambulizi hayo yataendelea.

Alithibitisha kuwa miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa Jumamosi jioni ni vituo viwili vya mafuta vinavyotumiwa kwa matumizi ya kawaida na ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na kusaidia shughuli za nyuklia.

Rais Trump amepongeza hatua za Israel katika mashambulizi hayo, huku akikanusha madai ya Iran kwamba Marekani imehusika moja kwa moja katika mashambulizi hayo.

Ametoa onyo kali kwa Iran kuhusiana na mpango wowote wa kupanua vita vyake vya kulipa kisasi kwa kuvishambulia vituo au mali za Marekani.

“Ikiwa tutashambuliwa kwa namna yoyote ile na Iran, nguvu kamili ya majeshi ya Marekani itashuka juu yenu kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa,” Trump aliandika katika ukurasa wake wa Truth Social. “Hata hivyo, tunaweza kufanikisha makubaliano kati ya Iran na Israel na kumaliza umwagaji huu wa damu kwa urahisi.”

Marekani imekuwa ikijaribu kujadiliana na Iran ili kuizuia kuendeleza mpango wake wa nyuklia, ambao Iran inasisitiza kuwa ni wa kiraia pekee, lakini Israel inaona kuwa ni tishio kubwa la kimaisha kwa sababu ya uwezekano wake wa kubuni silaha za nyuklia.

Hata hivyo, Trump hakutoa maelezo yoyote kuhusu makubaliano yanavyowezekana.