Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Treni ya mzigo ya SGR kuanza kesho

Muktasari:

  • Kwa kuanza kutakuwa na treni moja kila siku itayokuwa inaondoka Pugu saa 10 alfajiri na kusimama Morogoro saa 12:00 asubuhi na kufika saa 8:05 mchana ili kupisha treni za abiria.

Dar es Salaam. Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza kuanza huduma ya usafirishaji mizigo kwa njia ya reli ya kisasa ya SGR kati ya Pugu jijini Dar es Salaaam na stesheni ya lhumwa, Dodoma.

Reli hiyo ya SGR kwa sasa inaendelea kutumiwa na abiria pekee kati ya Dar es Salaam na Dodoma ambapo tangu Juni 14, 2024 ilipoanza kutoa huduma hadi Juni 2025 zaidi ya abiria milioni 2.5 wamesafirishwa.

Leo Alhamisi, Juni 26, 2025, TRC imetoa taarifa kwa umma ikieleza treni hiyo ya mizigo itaanza kasi kesho Ijumaa Juni 27.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TRC, Fredy Mwanjala imeeleza kwa kuanza kutakuwa na treni moja kila siku itakayokuwa inaondoka stesheni ya Pugu saa 10 alfajiri na kusimama Morogoro saa 12:00 asubuhi ili kupisha treni za abiria.

"…Baadaye kuendelea na safari ya Dodoma ambapo inatarajiwa kufika saa 8:05 mchana. Matarajio ni kuongeza idadi ya treni na mabehewa siku zijazo ili kuhudumia shehena nyingi zaidi," amesema Mwanjala.

Desemba 25, 2024 TRC ilitangaza kupokea shehena ya mabehewa 264 yaliyotengenezwa yaliyotengenezwa nchini China.

Taarifa iliyotolewa na Mwanjala ilieleza kati ya mabehewa hayo, 200 yatatumika kubeba makasha (makontena) na 64 yatabeba mizigo isiyofungwa.

“Mabehewa hayo yatakuwa yanatembea kwa kasi ya kilomita 120 kwa saa na majaribio yakikamilika, watalaamu wa TRC na wale wa mkandarasi wakijiridhisha mabehewa hayo yamekidhi viwango kwa mujibu wa mkataba, tarehe rasmi ya kuanza kazi itatolewa,” amesema.

Kwa mujibu wa Mwanjala, shehena ya mabehewa 264 yaliyowasili ni sehemu ya jumla ya mabehewa 1,430 ambayo kwa mujibu wa mkataba yanatengenezwa na Kampuni ya CRRC ya China.