Waliojenga daraja la Magufuli, SGR, kuwadhamini kimasomo wanafunzi wa uhandisi UDSM

Muktasari:
- Makubaliano ya miaka mitano yatawagusa wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza na shahada ya uzamili.
Dar es Salaam. Kampuni tatu kutoka nchini China zilizotekeleza miradi mbalimbali mikubwa hapa nchini, zimeingia makubaliano ya ushirikiano na chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kwa ajili ya kuwadhamini kimasomo wanafunzi wanaosemea fani za uhandisi na ujenzi chuoni hapo.
Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye, amesema makubaliano hayo ni ya miaka mitano na yatawagusa wale wanaosoma shahada ya kwanza na shahada ya uzamili katika masomo hayo.
Amesema ufadhili huo utaanza mwaka wa masomo 2025/26 huku vigezo vitakavyotumika ni kwa na ni kwa ambao wanefaulu vizuri masomo yao.
‘Tumekuwa na utaratibu wa siku nyingi wa kushirikiana na wenzetu ambao wako kwenye ajira na ambao wanatoa ajira au wameajiri watu ambao sisi tunawazalisha.
“Hivyo leo tulikuwa tunasaini mikataba kadhaa ya kampuni za kichina ambazo ziko tayari kutoa nafasi kwa wanafunzi wetu kuwasomesa kwa kutoa fedha,”amesema Profesa Anangisye.
Ukiacha udhaamini wa masomo, Makamu huyo amesema pia kampuni hizo zitawapa nafasi za mafunzo kwa vitendo wanafunzi hao ukizingatia kwa sasa serikali imekuwa ikisisitiza mafunzo ya amali, hivyo watamaliza wakiwa tayari na ujuzi.
Kampuni hizo zilizosaini makubaliano hayo ni KZJ New Materials Group, JUYE Concrete na CRJE (East Africa) Ltd zote kutoka nchini Nchini.

Meneja Mkuu wa kampuni ya KZJ Group, Dk Ma Xiuxing, amesema kampuni yao hiyo imeshiriki katika miradi ya miundombinu mbalimbali ikiwemo daraja la Magufuli, daraja la Tanzanite, Uwanja wa michezo wa Samia, sehemu ya uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme(LOTS 5 na LOTS 6).
Ujenzi mwingine walioshiriki kampuni hiyo, Dk Xiuxing amesema ni wa uwanja wa ndege Dodoma, upanuzi wa Bandari ya Tanga na Dar es Salaam na uwanja wa ndege wa Zanzibar.
“Wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo, kama kampuni tumegundua uwepo wa uhaba wa wataalam wa ndani na teknolojia duni katika miundombinu ndio maana tukaja na wazo hili la kuwadhamini kimasomo wanafunzi wanaosmoa hapa..
“Kwani kuna usemi usemao kumlisha mtu samaki ni kumshibisha kwa siku moja lakini kumfundisha ni kumshibisha katika maisha yake yote, na sisi ndio maana tumeona tuwafundishe wanafunzi wetu hawa ili ujuzi huo uwafai maishani,”amesema Meneja huyo.
Naye Naibu Meneja Mkuu wa kampuni ya wa CRJE(Afrika Mashariki), Bai Haochem, amesema kwa makubalinao hayo wanatumaini kuhamisha uzoefu wa teknolojia ya China ya muda mrefu kwa wahandisi wa Tanzania ili kuwasaidia kujifunza na kumiliki ujuzi wa hali ya juu.
Amesema CRJJE ndio kampuni inayofanya maboresho ya reli ya Tazara, imejenga daraja la Nyerere, na kukarabati uwanja wa ndege wa Kilimanjaro.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa kampuni ya JUYE Concret, Xu Honjuan, amesema wanaamini kupitia juhudi zao hizo , Tanzania itaangaza zaidi na urafiki kati ta yao na China utaendelea kuimariika na kusonga mbele.