Wasanii wa Hip Hop waliongiza fedha nyingi 2021

Muktasari:
- Katika orodha ya wasanii 10 wa Hip Hop walioingia fedha nyingi kwa mwaka 2021, Jay Z ameshika namba moja kuingiza Dola470 milioni ambazo ni tofauti ya Dola220 milioni na anayemfutia katika nafasi ya pili.
Katika orodha ya wasanii 10 wa Hip Hop walioingia fedha nyingi kwa mwaka 2021, Jay Z ameshika namba moja kuingiza Dola470 milioni ambazo ni tofauti ya Dola220 milioni na anayemfutia katika nafasi ya pili.
Hiyo ni kwa mujibu wa orodha iliyoandaliwa na Mhariri wa muda mrefu wa Forbes, Zack O'Malley Greenberg ambayo ilitoka Jumanne ya wiki hii ukiwa ni utaratibu wake wa kufanya hivyo kila mwaka.
Jay Z ajipatia fedha hizo baada ya kuuza hisa zake nyingi za mtandao wa Tidal kwa kampuni ya Square Inc kwa Dola302 milioni, huku fedha nyingine zikitokana na kampuni ya LVMH kununua nusu ya hisa za kinywaji chake, Armand de Brignac.
Kufuatia mafanikio hayo kwa mwaka 2021, utajiri wa Jay Z umeongezeka hadi kufikia Dola1.5 Bilioni, ikiwa ni miaka mitatu tangu alipotangazwa na Forbes kama msanii wa kwanza wa Hip Hop dunia kufikia hadhi ya Ubilionea.
Kanye West ambaye ameshika nafasi ya pili kwa kuingiza Dola250 milioni, fedha zake nyingi amezipata kwa kuuza bidhaa zake za Yeezy, huku Wiz Khalifa aliyeshika nafasi ya tano kwa Dola45 milioni akiingiza sehemu ya fedha hizo kwa biashara yake ya bangi, Khalifa Kush. Orodha kamili chini;
1. Jay Z – Dola470 milioni
2. Kanye West – Dola250 milioni
3. Diddy – Dola75 milioni
4. Drake – Dola50 milioni
5. Wiz Khalifa – Dola45 milioni
6. Travis Scott – Dola38 milioni
7. DJ Khaled – Dola35 milioni
8. Eminem – Dola28 milioni
9. J. Cole – Dola27 milioni
10. Birdman – Dola25 milioni
10. Doja Cat – Dola25 milioni
10. Tech N9ne – Dola25 milioni