Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Penzi la staa Bongo lilivyomtokea Savanna puani

Dar es Salaam. Wakati baadhi ya watu wakidhani anachokifanya Savanna Benson ‘Rais wa First Year’ ni maudhui tu. Mtengeneza maudhui hayo ya mtandaoni anasema kila anachokifanya kwenye mitandao, kina akisi maisha yake ya uhalisia.

Savanna amesema licha ya umaarufu wake, anapitia changamoto kwenye mahusiano kila kukicha.

Savanna ambaye amekuwa akitengeneza maudhui yanayozungumzia mahusiano, ameyasema hayo leo Aprili 8, 2025 wakati Pizza Hut Tanzania ikitangaza ushirikiano na kampuni ya Pepsi kuwa mtoa huduma pekee wa vinywaji katika maeneo yote ya Pizza Hut nchini.

"Kwanza mimi ni mtu napigwa matukio sana. Na siachani nayo mahusiano kwa sababu yananipa maudhui. Mara nyingi maudhui yangu ni maisha ya kweli naweza nikaongea kitu, watu wanacheka lakini kweli kipo.

"Mimi nakuwa kwenye mahusiano na mtu wa aina yoyote, awe maarufu au asiwe. Kuna mtu maarufu alinipiga matukio, tuliachana baada ya mimi kugundua ana mwanamke mwingine. Huwezi kuniona nagombania mpenzi kwa sababu wanaume wanaaibisha," amesema.

Amesema hata yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii yakimhusisha mwanamuziki Zuchu kurushiana maneno na aliyekuwa mpenzi wa Diamond, Rita Norbeth ni vyema wawili hao wangeachana nayo.

"Sitaki kuchagua upande wowote, lakini napenda kumwambia Zuchu anyamaze kwa sababu yule dada (Rita) sidhani kama amefikia viwango vyake. Zuchu ni mchapakazi mzuri na ana ushawishi kwa wanaweke wengi. Mwisho wa siku unagombana na mtu ambaye hana cha kupoteza," amesema

Licha ya hayo Savanna amesema hawezi kuwa na mwanaume mwenye tabia hizi;

"Siwezi kuwa na mwanaume ambaye anajiposti sana kwenye mitandao ya kijamii, utafikiri amepotea. Mwanaume ambaye hajitambui, anavaa kama mtoto anachanganya rangi. Lakini napenda mwanaume asiyeongea sana, kwa sababu mimi tayari naongea, lakini pia hela ni kigezo cha kwanza," amesema.

Utakumbuka hivi karibuni Savanna alitikisa mitandao ya kijamii, baada ya kuweka wazi kuwa amenunua gari aina ya BMW

"Nilivyonunua gari baadhi ya watu wanadai nitawaonyesha aliyeninunulia gari. Hiyo inaonyesha jamii yetu haiamini katika mtoto wa kike na haijui nguvu ya digital (mitandao). Napenda kusema Tiktok imeibua vipaji vingi sana.

"Kuna ile unaingia live unapata zawadi, lakini pia imefanya vijana wengi wapate namba kwa sababu ni mtandao ambao ni rahisi kufanya hivyo ni tofauti na Instagram ambapo mpaka ufanye kitu ndiyo watu wajue. Vitu ambavyo mtu anatakiwa kuwa navyo ili awe mtengeneza maudhui ni kamera nzuri, simu yenye uwezo wa kurekodi vizuri, confidence na ubunifu," amesema.

Awali wakitangaza makubaliano hayo, Meneja Masoko kutokea SBC Tanzania Limited Jasper Maston amesema ushirikiano huo ni nafasi ya kufikia wateja ambao wanapenda kufurahia chakula.

"Muunganiko huu unalenga mteja kupata huduma nzuri, lakini pia mpira ni njia moja wapo ambayo sisi tunaitumia kama wachezaji kwa sababu tunadhamini UEFA Champions League.

“Hata tukipata nafasi ya kudhamini league ya ndani mtaweza kuona utumiaji wa wachezaji wa ndani, hatujapata bado nafasi na mnavyojua Tanzania kuna wapenzi wengi wa mpira lakini tunapenda kuwa sehemu ya league ya Tanzania pia," amesema Jasper.

Naye meneja rasilimali watu na utawala kutoka kampuni ya Dough Works Limited Sixbert Mallya amesema lengo lao ni kuhakikisha Watanzania wananufaika na ushirikiano huo

"Tunavyoungana tunaweka wigo mpana tunatarajia mengi, na ushirikiano huu utakuwa wa muda mrefu," amesema Mallya.