Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mdogo wa marehemu Carina asimulia alichoambiwa na dada yake kwa mara ya mwisho

Dar es Salaam. Mdogo wa marehemu Hawa Hussein (Carina), Saphinewi Salvan amesema dada yake alimuahidi akirudi nchini atawaasili (adopt) watoto wake kisheria.

“Tarehe 14 tuliongea sana kila wakati alikuwa ananipigia simu. Alikuwa anasema mimi nataka leo tuongee, tukawa tunaongea video call akawa amesimama anapika. Ananiambia leo nataka kula chakula ambacho nimekipika mwenyewe.

"Nikamsifia amependeza, amekuwa mzuri sana. Akaniambia rangi yangu ni nzuri sana labda nakufa utajuaje, nikamwambia acha maneno yako bwana. Akaniambia nikirudi nataka niwaasili watoto wako kisheria sitaki uniingilie kwenye malezi yangu," amesema Saphinewi.

Mdogo huyo wa marehemu aliendelea kuonesha majonzi yake kwa kudai huenda angekuwa karibu na dada yake  angemuwahisha hospitali.

"Najuta kwanini nilirudi, natamani ningekuwepo ningemwambia dada yangu twende hospitali, labda angenikubalia kwa sababu waliokuwepo naye, wanasema tulikuwa tunamwambia tumpeleke hospitali lakini aliwaambia wataenda saa 1,” amesema.

Carina ambaye alifariki dunia Aprili 15, 2025 nchini India alipoenda kupatiwa matibabu, ameacha mtoto mmoja wa kike aitwaye Aisha mwenye umri wa miaka 16.  Mwili wa Carina utapumzishwa Jumamosi Aprili 19, 2025 kwenye makaburi ya Kisutu.

Utakumbuka Carina alionekana kama Video Queen kwenye wimbo wa ‘Oyoyo’ wa kwake Bob Junior lakini pia alicheza kwenye tamthilia ya kwanza ya mwigizaji Jacob Stephen ‘JB’ ya mwaka 2017 hadi 2018 iliyoitwa ‘Kiu ya Kisasi’.