Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usiyofahamu kuhusu safari ya Hashim Kambi

Mwigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Hashim Kambi enzi za uhai wake. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Enzi za uhai wake Kambi alipokua akifanya mahojiano na Mwananchi kuhusu safari yeke kwenye sanaa alisema mtu anayemuheshimu na kumuona kama baba yake ni Richie Richie (Single Mtambalike)

Dar es Salaam. Ni wazi kuwa yapo mengi aliyofanya marehemu Hashim Kambi kwenye kiwanda cha Bongo Movie. Lakini enzi za uhai wake hakusita kumtaja Richie Richie kama mtu aliyemuingiza kwenye sanaa hiyo. Twende pamoja

Enzi za uhai wake Kambi alipokua akifanya mahojiano na Mwananchi kuhusu safari yeke kwenye sanaa alisema mtu anayemuheshimu na kumuona kama baba yake ni Richie Richie (Single Mtambalike).

Mwigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Hashim Kambi enzi za uhai wake. Picha na Mtandao

Kambi alisema siku moja akiwa katika shughuli zake za biashara alikutana na msanii huyo na kumueleza namna gani anapenda kuigiza.

“Nilimueleza Richie namna nilivyokuwa nikivutiwa na uigizaji wake na ule wakina Natasha na Jacob Steven kwenye tamthiliya ya ‘Mambo Hayo’ hivyo nikamuomba kama naweza kupata nafasi ya kuigiza.”

Mwigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Hashim Kambi enzi za uhai wake. Picha na Mtandao

“Richie kwa kuwa tulijuana kwenye mashabiki wa timu ya Yanga, nilipomwambia hivyo ilikuwa rahisi na hapo ndio akampigia simu baba Haji na kumueleza kuwa wamepata mtu wa kucheza nafasi ya Benjamini katika tamthiliya ya ‘Uhondo wa Ngoma,” alisema

Tamthiliya hiyo ilikuwa ikiigizwa na wasanii kutoka kundi la maigizo la Kamanda Arts Family chini ya uongozi wake Haji Adam maarufu ’Baba Haji’ na kurushwa katika kituo cha TVT enzi hizo ambapo kwa sasa inajulikana kwa jina la Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC).

Single Mtambalike aliyemuingiza Kambi kwenye uigizaji

“Humo nilipewa nafasi ya kucheza kama Mzee Benjamin aliyekuwa tajiri katika hadithi ya tamthiliya hiyo na kujikuta nakuwa maarufu na kupata kazi nyingi za kufanya za filamu.

“Ni kutokana na Richie kunifungulia njia huko mpaka sasa hivi nimeweza kuwa msanii mkubwa na ninayeheshimika namshukuru kwa hilo na kwani huwa namuita baba yangu wa sanaa,” aliwahi kusema Kambi wakati akisimulia safari yake.