Hashim Kambi afariki dunia, chanzo chatajwa
Mwigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Hashim Kambi enzi za uhai wake. Picha na Mtandao
Muktasari:
- Msanii Mkongwe wa Bongo Movie Hashim Kambi amefariki dunia leo April 27, 2026. Kwa maradhi ya presha.
Dar es Salaam. Tasnia ya filamu nchini imepata pigo kufuatia kifo cha mwigizaji mkongwe wa Bongo Movie, Hashim Kambi, aliyefariki dunia leo Aprili 27, 2026, baada ya kusumbuliwa na maradhi ya presha.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa leo Jumatatu Aprili 27, 2026 na Msemaji wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Coletha Raymond, amesema kuwa msanii huyo alizidiwa ghafla akiwa kazini katika eneo la Pilipili.
"Alikuwa kazini pale Pilipili kwa taarifa nilizonazo akazidiwa. Wakamkimbiza hospitali kwa sababu Pilipili na Mico ni sehemu karibu. Alipofika wakati wanahangaika kumsaidia umauti ukamkuta.
"Na kilichomuua ni presha sasa na mimi naenda kuungana nao. Waliopo pale wanahangaika kumtoa pale kumpeleka Muhimbili. Msiba bado sijajua utakuwa wapi ingawa familia yake na mkwe wake wanaishi Tabata," amesema Coletha