Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msanii Spack afariki dunia, meneja afunguka ilivyokuwa kabla ya kifo

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwananchi meneja wa msanii huyo Abdulrahman Hassan 'Malefti' amesema jana alizungumza na msanii huyo kuhusu mpango wao wa kushoot video ya wimbo mpya.

Dar es Salaam. Mwanamuziki wa zamani wa Bongo Fleva Selemani Ramadhani Mvamba 'Spack' amefariki dunia leo Aprili 27,2026.

Akizungumza na Mwananchi meneja wa msanii huyo Abdulrahman Hassan 'Malefti' amesema jana alizungumza na msanii huyo kuhusu mpango wao wa kushoot video ya wimbo mpya.

"Ni kweli amefariki mara ya mwisho nimezungumza nae saa saba usiku. Akaaga akaenda kulala sasa asubuhi alienda kugongewa kwa ajili ya kutoa nauli za watoto kwenda shule.

"Akawa haamki, jana tulivyozungumza alikuwa mzima alinitumia wimbo akasema niusikilize kwa sababu leo tulikuwa tunaenda Sinza kukutana na director Lenzo kwa ajili ya kuandika script za video ya wimbo wake mpya,"amesema meneja

Meneja huyo ameongezea, jana usiku walizungumza masuala ya kazi kwa furaha bila kuonesha dalili yoyote ya kuumwa.

"Alikuwa akiishi na mwanamke wake ingawa na yeye kwa muda anaumwa. Kwahiyo alienda kwao, nyumbani Spack alibaki na watoto na mfanyakazi. Msiba utakuwepo Chamazi kwa Mkongo ndipo alipo baba yake kwa sasa na baadhi ya kaka zake. Taratibu zilizopo hapa ni kuuhamisha mwili na kuupeleka Chamazi. 

"Tangu nianze kufanya nae kazi nafahamu ana watoto wanne, wawili mapacha wapo kwa mama yao Kariakoo na wengine wawili alikuwa akikaa nao. Mmoja yupo darasa la nne na mwingine darasa la kwanza,"amesema meneja Malefti

Hatahivyo Malefti amesema baada ya yaliyotokea majirani walimpeleka hospitali ya Nguvu Kazi iliyopo Chanika. Ambapo ndipo daktari alithibitisha kuwa msanii huyo amefariki dunia