Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuhuma za ubakaji zilivyomkosesha Jay Z mamilioni ya dola

Muktasari:

  • Mkali huyo wa kibao, Run This Town (2009), anadai kuwa mshtaki wake [Jane Doe] hajaacha kutoa kauli za kashfa kumhusu ingawa alikubali kufanya hivyo. Anadai kauli hizo zimemgharimu yeye na kampuni yake Roc Nation kwa kupoteza mamilioni ya dola.

Marekani. Licha ya kesi ya ubakaji iliyokuwa inamkabili Jay Z kutupiliwa mbali tangu Februari, bado rapa huyo anadai haki yake ambapo wiki hii mawakili wake wamewasilisha kesi huko Alabama wakidai mteja wao kuchafuliwa na tuhuma hizo.

Mkali huyo wa kibao, Run This Town (2009), anadai kuwa mshtaki wake [Jane Doe] hajaacha kutoa kauli za kashfa kumhusu ingawa alikubali kufanya hivyo. Anadai kauli hizo zimemgharimu yeye na kampuni yake Roc Nation kwa kupoteza mamilioni ya dola.

Ikumbukwe Oktoba 2024, Jane Doe, 37, aliwashtaki Jay Z na Diddy kwa madai kuwa mwaka 2000 alipokuwa binti wa miaka 13, wasanii hao walimbaka mara baada ya kumalizika hafla ya ugawaji wa tuzo za MTV VMAs.

Hata hivyo, Februari mwaka huu kwa hiari yake Doe aliamua kuifuta kesi hiyo na ndipo rapa huyo wa Brooklyn akachukua uamuzi wa kumshtaki wakili wake, Tony Buzbee kwa makosa ya unyang’anyi na kumchafua.

“Kesi ya uongo dhidi ya Jay Z ambayo kamwe haikupaswa kusikilizwa, imetupiliwa mbali,” alisema wakili wake Alex Spiro wakati huo na kuongeza.

“Kwa kusimama kidete dhidi ya madai ya uongo, Jay Z amefanikisha kile ambacho wengi wameshindwa. Hajarudi nyuma wala hajalipa hata senti moja ili kulisafisha jina lake,” alisema Spiro.  

Katika jalada lake jipya, Jay Z anadai kwamba mnamo Aprili 11, Doe alichapisha video TikTok ambayo ililenga kuwapotosha watazamaji kuwa Jay Z alijaribu kumlipa fedha nyingi ili amuombe msamaha kwa mashtaka aliyomfungulia hapo awali.

Mtandao wa Rolling Stone umepata malalamiko ya Jay Z ambayo yanaeleza kwa nini vitendo vya Doe vinaathiri biashara yake kwa kupoteza fursa nyingi za kibiashara.

“Kutokana na washtakiwa kuwasilisha kesi ya uongo na taarifa nyingine za uongo kwa umma dhidi ya Bw. Carter [Jay Z], walimkosesha fursa ya kupata mkopo binafsi wa Dola55 milioni.  Pia Roc Nation ilinyimwa mkopo wa Dola 115 milioni,” taarifa ilieleza.  

Baada ya kushtakiwa mwaka uliopita, Jay Z kupitia Roc Nation alikanusha madai hayo na kusema yeye sio kama watu wengine maarufu, amekuwa akiwalinda watoto na kuyaita madai hayo ya kipuuzi na yenye lengo la kupata aina fulani ya faida kama fedha.

Rapa Soulja Boy aliibuka na kumtetea Jay Z kwa kukosoa kile alichoita jitihada za kuharibu alama iliyowekwa kwa umma na watu maarufu wa rap na kusema hayupo tayari kuona anarudishwa nyuma kwa mambo kama hayo.

“Ukiwa katika hii tasnia na kusimama kama biashara wataanza kuchafua jina lako, watajaribu kukushusha, hawataki kuona tunashinda na hawataki kuona tuna hizi fedha. Unapokuwa katika tasnia hii ya rap na kuwa mtu mashuhuri, utalengwa tu,” alisema Soulja Boy.

Tangu katikati mwa miaka ya 1990, Jay Z amekuwa na ushawishi katika muziki huku akifungua biashara nyingi ambazo zilimfanya kuwa msanii wa kwanza Hip Hop duniani kufikia hadhi ya ubilionea.

Mwaka 2008, ndipo alianzisha kampuni ya Roc Nation ikiwa imejikita kutoa huduma katika tasnia burudani kama wakala wa usimamizi wa wasanii na imeshafanya kazi na wasanii kama J. Cole, Rihanna, DJ Khaled, Kelly Rowland, Alicia Keys n.k.

Ikiwa na makazi yake New York na Los Angeles, Marekani pamoja na London, Uingereza, vilevile Roc Nation inasimamia wanamichezo chini ya Roc Nation Sports, na pia inajishughulisha na utayarishaji filamu, vipindi vya televisheni n.k.