Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siku 182 za heshima kwa mastaa Bongo

Muktasari:

  • Kwa takribani siku hizo 182, wasanii hao kwa mara ya kwanza wamefanya au kukutana na matukio kuanzia ngazi ya familia, biashara na sanaa ambayo yamewaongezea heshima kubwa katika tasnia na mbele ya mashabiki wao

Dar es Salaam, Wasanii kama Harmonize, Alikiba na Monalisa ni miongoni mwa mastaa Bongo ambao wamepata heshima kubwa tena ya kipekee ndani ya kazi zao katika nusu ya mwaka 2024 ambayo imekamilika hivi karibuni.  

Kwa takribani siku hizo 182, wasanii hao kwa mara ya kwanza wamefanya au kukutana na matukio kuanzia ngazi ya familia, biashara na sanaa ambayo yamewaongezea heshima kubwa katika tasnia na mbele ya mashabiki wao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye tangu ameingia madarakani ameonekana kuiunga mkono sanaa, naye ni sehemu ya waliowaheshimisha wasanii hao.

Tunasema nusu ya mwaka 2024 imewaheshimisha kwa sababu tangu wasanii hao wameanza sanaa hawakuwahi kufanya au kukumbana na fursa kama walizozipata kwa kipindi hicho. Miongoni mwa hayo, ni haya yafuatayo.

Kwa Samia, baada ya Sugu ni Harmonize
Staa wa Bongo Fleva, Harmonize ni msanii wa kwanza Tanzania kwa albamu yake kuzinduliwa na Rais Samia, tukio lilofanyika Mei 25 Mlimani City, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, wasanii, mashabiki na wadau.

Albamu hiyo aliyoipa jina la ‘Muziki wa Samia’ imejikita kueneza uelewa kwa wananchi kuhusu yale yaliyofanywa na Rais Samia tangu kuingia madarakani miaka mitatu iliyopita akiwa ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.

Harmonize ambaye albamu yake ya kwanza ilizinduliwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete hapo Machi 2020, hadi sasa tayari ametoa albamu tano, Afro East (2020), High School (2021), Made For Us (2022), Visit Bongo (2023) na Muziki wa Samia (2024).

Ikumbukwe Mei 31, 2022 Rais Samia alikuwa mgeni rasmi katika tamasha la mkongwe wa Hip Hop, Mr. II Sugu, The Dream Concert ambapo alizundua kitabu cha Sugu ‘Muziki na Maisha’ pamoja na kumpatia tuzo kwa kutimiza miaka 30 katika muziki.


Marioo, Paula wazazi wapya mjini
Wakiwa wanatimiza mwaka mmoja wa uhusiano wao, Marioo na Paula alitangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza baada ya tetesi za muda mrefu ambazo wenyewe kila mara walikuwa wanakwepa kuzizungumzia.  

Paula ambaye uhusiano wake na Marioo ulianza kuangaziwa na mitandao na vyombo vya habari tangu Aprili 2023, alijifungua mtoto wa kike hapo Mei 3 na kumpa jina la Amarah ingawa walikuja kutangaza jambo hilo katika mitandao mnamo Mei 21,

“Nataka tu kusema asante Mungu, moyo wangu umejaa na shukrani. Asante Amarah kwa kunichagua kuwa mama yako, Mungu alijua moyo wangu unakuhitaji.” alisema Paula, binti wa P-Funk Majani na Kajala Masanja.

Utakumbuka tangu Marioo ametoka kimuziki na wimbo wake, Dar Kugumu (2018), Paula ndiye mrembo pekee aliyetokea katika video nyingi za nyimbo zake ambazo ni Lonely (2023), Tomorrow (2023), Sing (2023) na Hakuna Matata (2024).

Baada ya N’Dour na Diamond, ni Alikiba
Akiwa anasherekea kutimiza miaka 20 katika Bongo Fleva, Alikiba aliamua kuheshimisha ukongwe wake katika muziki kwa kutambulisha kituo chake cha redio, Crown FM 92.1 kikisikika Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga na Pwani.

Redio hiyo ilizinduliwa Machi 9 katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa kama Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Mkuu wa Mkoa Dar, Albert Chalamila.

Alikiba anakuwa msanii wa pili wa Bongo Fleva kumiliki redio yake baada ya Diamond Platnumz mwenye Wasafi FM na Wasafi TV, huku Youssou N’Dour, mshindi wa Grammy 2005 kutoka Senegal akitajwa kuwa msanii wa kwanza Afrika kufanya hivyo.

Ikumbukwe Alikiba aliyevuma zaidi kimuziki baada ya kuachia albamu yake ya kwanza, Cinderella (2007) chini ya G Records, pia ni mmiliki wa Kings Music, rekodi lebo inayowasimamia wasanii kama Tommy Flavour, K2ga, Abdukiba na Vanillah.

Monalisa, Lulu safarini na Rais hadi Korea
Akiwa katika uzinduzi wa albamu ya Harmonize, Rais Samia alitangaza kuanza kusafiri na wasanii katika ziara zake za nje ili kuwapa fursa ya kujifunza zaidi kwa wenzao na kuja kuinua tasnia ya burudani nchini.

Katika ziara yake nchini Korea Kusini iliyoanza Mei 31, Rais Samia aliongozana na baadhi ya waandaaji wa filamu na waigizaji wa Tanzania ambao walikutana na wenzao wa huko katika jijini la Seoul ili kujifunza.

Miongoni mwa mastaa waliopata fursa hiyo ni Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Monalisa na Lamata ambaye ni muandaaji wa tamthilia ya Jua Kali na Kapuni.