Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rema bado yupo sana Mavin Records

Muktasari:

  • Hapo awali kulikuwa na uvumi kuwa Rema aliyetamba na Wimbo Calm Down (2022) ameachana na Mavin Records na kampuni tanzu yake, Jonzing World ambayo inamilikiwa na kaka yake Don Jazzy, D’Prince.

Nigeria, Mtayarishaji wa muziki kutoka Nigeria ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mavin Records, Don Jazzy amekanusha tetesi kuwa mwimbaji maarufu Afrika, Rema amevunja mkataba wake na rekodi lebo hiyo.

Hapo awali kulikuwa na uvumi kuwa Rema aliyetamba na Wimbo Calm Down (2022) ameachana na Mavin Records na kampuni tanzu yake, Jonzing World ambayo inamilikiwa na kaka yake Don Jazzy, D’Prince.

Utakumbuka Rema alianza muziki katika makanisa ya Alpha P, chapisho lake la video katika Mtandao wa Instagram akiimba Wimbo wa D’Prince, Gucci Gang lilivutia usikivu wa D’Prince na kumsafirisha hadi Lagos na kumpa Rema ofa ya kujiunga Jonzing World.

Hivi karibuni Don Jazzy kupitia mitandao ya kijamii amezima tetesi hizo baada ya kuchapisha picha yake akiwa na Rema pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Mavins Records, Tega Oghenejobo na kuandika “Mavins in Paris”.

                      

Rema na uongozi wake wakiwa Paris

Chapisho hilo lilikuja siku chache baada ya Rema kutumbuiza kwenye Tamasha la Yardland huko Paris, Ufaransa hapo Julai 7, 2024 akiwa na wasanii wengine kutoka Nigeria kama vile Odumodublvck.

Don Jazzy amedokeza kwamba Rema anaendelea kuwa sehemu ya familia ya Mavin Records, hatua ambayo imewatuliza mashabiki wa lebo hiyo na muziki wa Rema ambaye alitoka kimuziki kupitia wimbo wake, Dumebi (2019).

Mavins Records iliyoanzishwa Mei 2012 ikianza na wasanii kama Tiwa Savage, Wande Coal, Reekado Banks na Iyanya, kwa sasa inawasimamia kina Rema, Ayra Starr, Crayon, Johnny Drille, Ladipoe, Magixx, Boy Spyce, Bayanni na Lifesize Teddy.

Chini ya Jonzing World na Mavins Records, Rema amepata mafanikio makubwa kimuziki, mathalani remix ya wimbo wake, Calm Down (2022) akimshirikisha Selena Gomez, video yake imefikisha ‘views’ zaidi ya milioni 900 YouTube.

Pia wimbo huo ulishinda Tuzo ya MTV Video Music 2023 huko Marekani kama Wimbo Bora wa Afrobeats na Rema kusema alijua wimbo ungefanya vizuri na kumshukuru Selena kwa kushiriki katika kazi hiyo.

“Ninaamini kuwa kila kitu ninachofanya ni maalum, nyimbo tofauti zitasikika kwa watu tofauti, nilipoingia studio kwa kweli nilikuwa nikiimba ukweli wangu, nilifanya kile ambacho nilipaswa kufanya.” alisema.

“Mimi na Selena tunazungumza mara kwa mara, sisi ni marafiki, hatujapata muda wa kukaa na kusherehekea mafanikio haya kwa sababu sote tunafanya kazi lakini bila shaka tutafanya hivyo.” Rema aliliambia Jarida la People.

Ikumbukwe albamu ya kwanza ya Rema, Rave & Roses (2022) ilifanya vizuri na kushika nafasi ya 81 kwenye chati za Billboard 200 huku wimbo wake ‘Calm Down Remix’ ukiweka rekodi ya kukaa katika chati za Billboard U.S Afrobeats Songs kwa wiki 58.