P Diddy, Diageo wamaliza tofauti zao

Muktasari:
- Kwa mujibu wa jarida la ‘People’ P Diddy na Diageo wamefikia makubaliano ya kumaliza tofauti zao na ‘rapa’ huyo amefuta mashitaka aliyofungua mahakamani.
Marekani. Baada ya kurindima mahakamani kesi iliyofunguliwa na ‘rapa’ kutoka Marekani P Diddy kwa kuishutumu kampuni ya vinywaji ya Diageo kwa ubaguzi wa rangi, hatimaye wamemaliza tofauti zao.
Kwa mujibu wa jarida la ‘People’ P Diddy na Diageo wamefikia makubaliano ya kumaliza tofauti zao na ‘rapa’ huyo amefuta mashitaka aliyofungua mahakamani.
Mei 2023, iliripotiwa kuwa P Diddy aliishitaki Kampuni ya Diageo kwa ubaguzi wa rangi, baada ya kampuni hiyo kutemana naye huku ikidai vinywaji alivyokuwa akitangaza ‘rapa’ huyo vilikuwa havifanyi vizuri sokoni kwa sababu alikuwa mtu mweusi.
Diddy amefanya kazi na kampuni hiyo kwa miaka 15, mara ya kwanza alianza mwaka 2007 akiwa anatangaza bidhaa zao, lakini mwaka jana walitemana na ndipo Diddy akafungua kesi dhidi ya kampuni hiyo.