Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lupita Nyong’o awapongeza Gen Z sakata la maandamano

Mwigizaji Lupita Nyong’o.

Muktasari:

  • Wananchi wa Kenya wameandamana kwa wiki ya pili mfululizo wakilalamikia muswada mpya wa fedha ambao ulipitishwa na Bunge.

Dar es Salaam. Mwigizaji Lupita Nyong’o, raia wa Kenya amewapongeza vijana wa ‘Gen Z’ na wananchi wote nchini humo kuandamana kupinga muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2024/25.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nyong’o ameweka ujumbe akiwashukuru wananchi kwa ujumla kujumuika kutetea haki zao, huku akiitaka Serikali ya Kenya kusikiliza ombi la wananchi wao na kulifanyia kazi.

“Ninawasalimu Wakenya na ninawashukuru sana kwa kujumuika pamoja, ili kusimama dhidi ya mswada wa sheria ya fedha kifedha ambao haupo sawa wa 2024 na pia kutetea na kukuza haki ya kidemokrasia ya watu wa Kenya.”

“Nina huzuni kubwa kwamba baadhi ya watu wamepoteza maisha katika mchakato huo, kwa maoni yangu naomba Serikali ya Kenya iliunganishe tena Taifa hilo kwa kusikiliza na kushughulikia matatizo yanayojitokeza”

Mkali huyo wa ‘Black Panther’ amewahi kuonekana katika filamu kama ‘Queen of Katwe’, ‘12 Years a Slave’, ‘A Quiet Place: Day One’ na nyinginezo.

Sio mwigizaji huyo tuu ambaye ameungamkono maanadamano hayo wapo mastaa mbalimbali kutoka Kenya waliungana na wananchi akiwemo Khaligraph, Joviali, Eric Omondi, Otile Brown na wengineo.

Vijana hao wa Gen Z wamefanya maandamano hayo kwa wiki ya pili mfululizo wakilalamikia muswada mpya wa fedha ambao ulipitishwa na Bunge.

Maandamano hayo yalienea karibu nchi nzima ya Kenya ambapo jana vijana hao waliingia ndani ya majengo ya Bunge na kuzua mvutano na polisi.