Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miswada sita kutinga mkutano Baraza la Wawakilishi Zanzibar

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Raya Issa Mselem akizungumza na waandishi  wa habari ( hawapo pichani) katika ukumbi wa mikutano wa  Baraza hilo Chukwani nje kidogo ya mji ya Zanzibar. Picha na Muhammed Khamis

Muktasari:

  • Mkutano huo wa 13 wa Baraza la Wawakilishi utaanza Jumatano pamoja na mambo mengine mwakilishi mteule wa jimbo la Mtambwe atakula kiapo cha utiifu.

Unguja. Jumla ya miswada sita inatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano wa 13 wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar utakaoanza Jumatano, Novemba 29, 2023.

Katika mkutano huo, kutafanyika shughuli mbalimbali ikiwemo kiapo cha uaminifu kwa mwakilishi mteule wa Jimbo la Mtambwe, Dk Mohamed Ali Suleiman kutoka Chama cha ACT-Wazalendo.

Hayo yameelezwa leo, Novemba 27, 2023 na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Raya Issa Mselem wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa baraza hilo Chukwani, nje kidogo ya mji wa Unguja.

Amesema miswada hiyo ni muswada wa sheria iliowasilishwa na kusoma kwa mara ya kwanza katika mkutano wa Septemba 2023, itasomwa tena kwa mara ya pili na kujadiliwa.

Miswada huyo ni wa sheria ya kuanzisha ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali namba 11 ya mwaka 2003 ya kutunga sheria ya ukaguzi wa umma na kuweka mambo mengine yanayohusiana na hayo.

Pia muswada wa sheria ya kufuta sheria ya Mahakama ya Kadhi namba 9 ya mwaka 2017 na kutunga sheria ya Mahakama ya Kadhi na kuweka mambo mengine yanayohusiana na hayo.

Kutakuwa pia na muswada wa sheria ya kuweka masharti ya utoaji leseni, kudhibiti na kusimamia biashara ya huduma ndogondogo  za fedha kwa ajili ya kudumisha utulivu, usalama na ubora wa huduma.

Amesema pia kutakuwa na muswada mwingine wa kufuta Sheria ya Mamlaka ya Kukuza na Kulinda Uwekezaji Zanzibar namba 14 ya 2018 na kutunga sheria ya uwekezaji Zanzibar.

Miswada mingine ni kuazishwa kwa taasisi ya utafiti wa uvuvi na maliasili za baharini Zanzibar pamoja na muswada wa kuanzishwa kwa wakala wa bohari kuu ya dawa  kwa ajili ya ununuzi, utengenezaji na uhifadhi na usambazaji pamoja na mambo mengine yanahusu dawa.

Amesema pia katika mkutano huo,  kutaulizwa maswali 88 kutoka kwa wajumbe na kupatiwa majibu ya Serikali.