Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huu hapa mchanganuo waliochukua fomu za ubunge, uwakilishi na udiwani Z’bar

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar,  Khamis Mbeto akizungumza na waandishi wa habari kuhusu makada wa chama hicho waliochukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania ubunge, uwakilishi na udiwani Zanzibar. Picha na Jesse Mikofu

Muktasari:

  • Kati ya waliochukua na kurejesha fomu 2089 katika majimbo 50 ya Uchaguzi na nafasi za makundi, wanawake ni 855. Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu ndani ya chama hicho ulianza Juni 28 hadi Julai 2, 2025.

Unguja. Makada 2092 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani huku watatu wakiingia mitini kurejesha fomu zao hivyo kufanya idadi ya waliochukua na kurejesha kuwa 2089 Zanzibar.

Kati ya hao wanawake waliochukua fomu na kurejesha katika makundi yote walikuwa 855, kati ya hao waliochukua fomu za majimbo ni 406.

Kwa upande wa wabunge pekee waliochukua fomu na kurejesha ni 485 huku upande wa uwakilishi wakiwa 400.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari makao makuu ya chama hicho Kisiwandui leo jioni Julai 3, 2025, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto amesema idadi hiyo inaonesha kukua kwa demokrasia ndani ya chama hicho na watu kuwa na Imani nacho kwani haijawahi kutokea wingi wa namna hiyo.

"Katika hatua hii pekee inaonesha wazi kwamba tunakwenda kushinda uchaguzi kwani Imani inazidi kuongezeka kwa chama chetu,” amesema Mbeto.

Kwa upande wa Wilaya ya Mjini yenye majimbo manne, waliojitokeza kuchukua na kurejesha fomu nafasi ya Ubunge ni 43 na uwakilishi 37 huku madiwani wakiwa 61 kwenye wadi nane.

Wilaya ya Amani yenye majimbo matano, nafasi ya ubunge 30 na uwakilishi 51 huku upande wa madiwani wakiwa 66 katika wadi 10.

"Katika Wilaya ya Mfenesini yenye majimbo matano, nafàsi ya ubunge 61 na uwakilishi 44 na madiwani ni 68," amesema Mbeto.

Kwa upande wa Wilaya ya Domani, nafasi za ubunge wamejitokeza 80 na uwakilishi 42 na madiwani ni watu 14 pekee.

Mbeto amesema katika Mkoa wa Kaskazini Unguja wamejitokeza jumla 328, kati ya hao Wilaya ya Kaskazini A yenye majimbo manne nafasi za wabunge ni 52 na uwakilishi 38 huku madiwani 67 katika wadi 10.

Wilaya ya Kaskazini B wamejitokeza makada 26 kwa nafasi za ubunge na 16 uwakilishi na madiwani 57 kwenye wadi Saba.

Kwa upande wa Mkao wa Kusini Unguja wamejitokeza makada 194 kwenye Wilaya mbili zenye majimbo matatu. Nafasi za ubunge 32 na uwakilishi 35.

Katika Wilaya ya Kusini Unguja kwa nafasi za ubunge na uwakilishi waefungana kwa idadi ya makada 13 kila upande huku madiwani wakiwa 24 katka wadi nne.

Mkoa wa Kusini Pemba, idadi ya watu waliojitokeza kuchukua fomu katika Wilaya zote mbili ni 385. Wilaya ya Chakeche Kwa nafasi za ubunge ni 51 na uwakilishi 25 huku madiwani wakiwa 98 katika wadi 10.

Kwa upande wa Wilaya ya Mkoani waliojitokeza kwenye ubunge ni 41 na uwakilishi 30 na upande wa madiwani ni 75 katika wadi 9.

Katika Mkoa wa Kaskazini Pemba wenye Wilaya mbili jumla ya walochukua fomu ni 306. Kwa wilaya ya Were nafasi za ubunge ni 27 na uwakilishi 44 huku madiwani wakiwa 68 kwenye wadi 10.

Mbeto amesema Wilaya ya Micheweni waliochukua fomu ubunge ni 29, na uwakilishi 25 nafasi za udiwani ni 51 kwenye wadi nane.

Amesema baada ya kukamilisha mchakato huo sasa unaanza mchakato wa vikazo vya ngazi za kamati ya siasa ya Jimbo kujadili majina hayo.