Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwalimu, Devotha waanza ziara mikoani kuomba udhamini

Muktasari:

  • Viongozi hao wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) wameanza ziara mikoa mbalimbali kujitambulisha na kuomba saini za wadhamini.

Dar es Salaam. Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu, ameanza rasmi ziara mikoani kujitambulisha na kutafuta  wadhamini.

Mwalimu ambaye ameambatana na mgombea mwenza wake, Devotha Minja, ameanza safari hiyo leo Jumamosi, Agosti 16, katika mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara) na baadaye  ataendelea katika maeneo mengine.

Msafara huo unaojumuisha viongozi waandamizi wa chama hicho kutoka makao makuu umeondoka alfajiri leo jijini Dar es Salaam kuelekea Lindi.

Chaumma, ni miongoni mwa vyama 18 vilivyoteua makada waliochukua fomu za kuwania kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

Baada ya kuhitimishwa kwa shughuli ya uchukuaji wa fomu hizo kutoka Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) jana Ijuma Agosti 15, 2025, sasa ni wakati kwa wagombea kuzunguka kutafuta saini za wadhamini katika mikoa isiyokupungua 10 ikiwemo miwili ya Zanzibar.