Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yazoa tuzo Ligi Kuu mwezi Desemba

Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Concalves. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Kocha Pedro Goncalves ameiongoza Yanga katika mechi tatu za Ligi Kuu ambazo zote imeibuka na ushindi.

Dar es Salaam. Yanga imetawala tuzo za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwezi Desemba ambapo imevuna tuzo mbili ambazo ni za Mchezaji Bora na Kocha Bora.

Kiungo Duke Abuya amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa huku Pedro Concalves akichaguliwa kuwa Kocha Bora. 

Duke alionesha kiwango kizuri chenye muendelezo akiisaidia timu yake kushinda michezo miwili iliyocheza mwezi huo, pamoja na kuhusika katika mabao mawili kwa dakika 180 za michezo hiyo.

Mchezaji huyo aliwashinda Nassor Saadun wa Azam na Prince Dube wa Yanga alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa upande wa Pedro aliyeingia fainali katika mchakato huo na Florent Ibenge wa Azam na Etienne Ndairagije wa TRA United, aliiongoza timu yake kushinda michezo miwili na kupaa kutoka nafasi ya nne hadi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Yanga ilizifunga Fountain Gate (2-0), na Coastal Union (0-1).

Wakati huohuo Meneja wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Said Mpuche, amechaguliwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Desemba kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Katika hatua nyingine mchezaji wa Transit Camp, Adam Uledi, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Desemba wa Ligi ya Championship huku Shadrack Nsajigwa pia wa Transit Camp akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Uledi aliyeingia fainali katika mchakato huo na Obrey Chirwa wa Kagera Sugar na Boniface Mwanjonde wa Mbeya Kwanza, alionesha kiwango chenye muendelezo ikiwa ni pamoja na kucheza dakika 450 za michezo mitano aliyocheza.

Kwa upande wa Nsajigwa aliyeingia fainali na Juma Kaseja wa Kagera Sugar na Zuberi Katwila wa Geita Gold aliwezesha timu yake kushinda michezo yote mitano iliyocheza mwezi huo.