Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yatibuliwa hesabu ikifungwa na Ahly

Muktasari:

  • Al Ahly ni mabingwa wa kihistoria wa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa wamelitwaa mara 12.

Dar es Salaam. Yanga imeshindwa kufua dafu ugenini huko Alexandria, Misri baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Al Ahly katika mechi ya raundi ya tatu ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Mabao mawili ya Mahmoud Hassan ‘Trezeguet’ yalitosha kuizamisha Yanga na kuipa Al Ahly ushindi ambao umeifanya ifikishe pointi saba na kuendelea kuongoza msimamo wa kundi B.

Bao la kwanza la Trezeguet alipachika katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa krosi wa Mohamed Hany.

Bao hilo lilidumu hadi filimbi ya kumaliza kipindi cha kwanza ilipopulizwa.

Dakika 12 baada ya kipindi cha pili kuanza, Yanga ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Mohamed Damaro na Israel Mwenda ambao nafasi zao zilichukuliwa na Pacome Zouzoua na Mudathir Yahya.

Al Ahly walijibu mapigo katika dakika ya 66 kwa kumtoa Marwan Attia na kumuingiza Nejc Gradisar huku Yanga katika dakika ya 75 wakimfanyia mabadiliko Allan Okello na kumuingiza Prince Dube.

Dakika hiyo ya 75 ambayo Dube aliingia, Al Ahly ilipata bao la pili kupitia kwa Trezeguet tena ambaye alifunga bao hilo kwa shuti la wastani alilopiga kwa staili ya kuzungusha mpira na kuujaza wavuni.

Baada ya kuingia bao hilo, timu hizo zilishambuliana kwa zamu, Al Ahly ikionekana kusaka mabao ya kuongeza huku Yanga ikionekana kuhitaji kusawazisha.

Hata hivyo ubao wa matokeo haukuweza kubadilika hadi filimbi ya mwisho ya mchezo ilipopulizwa.

Mabadiliko mengine ya wachezaji yaliyofanywa na Yanga katika mchezo huo ni ya kuwatoa Dickson Job na Chadrack Boka ambao nafasi zao zilichukuliwa na Yao Attohoula na Mohamed Hussein.

Al Ahly iliwatoa Emam Ashour, Ahmed Zizo, Trezeguet na Mohamed Hany ambao nafasi zao zilichukuliwa na Taher Mohamed, Hussein El Shahat, Mohamed Ben Romdhane na Ahmed Eid.

Ushindi huo umeifanya Al Ahly kuendelea kuongoza msimamo wa kundi B ikifikisha pointi saba.

Timu hizo sasa zitarudiana katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar, Januari 30, 2025.