Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yafukua mafaili ya Nabi

Muktasari:

  • Achana na kuishia kwao hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, jambo jipya kwa Yanga ni kuona wanatetea mataji yao ya ndani, Kombe la FA na Ligi Kuu Bara.

Yanga imeangalia mwenendo wa kikosi chao na kugundua kwamba kuna mambo madogo ambayo yakifanyiwa kazi basi watatisha zaidi msimu huu kwani kuna mwanga wameanza kuuona.

Achana na kuishia kwao hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, jambo jipya kwa Yanga ni kuona wanatetea mataji yao ya ndani, Kombe la FA na Ligi Kuu Bara.

Wanateteaje? Uongozi wa klabu hiyo umekaa na kocha Sead Ramovic na kuamua kurudisha utaratibu wa zamani ambao ulikuwa ukifanyika chini ya Nasreddine Nabi.

Nabi ambaye alikuwa kocha wa Yanga kuanzia Aprili 20, 2021 hadi Juni 15, 2023 wakati wake kikosini hapo timu ilikuwa ikikaa kambini muda mwingi tofauti na utawala wa aliyefuatia, Miguel Gamondi ambaye alianza hivyo, kisha ukabadilishwa.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zimebainisha kwamba, ule utaratibu wa kukaa kambini Avic umerejea na wanaanza leo wakijiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Copco utakaochezwa Jumamosi ya wiki hii Uwanja wa KMC Complex, Dar.

"Ni kweli timu ilikuwa inakaa kambini siku mbili hadi tatu kabla ya mchezo, kutokana na hilo kocha ameomba kuiona timu ikikaa kambini muda mrefu ili viwango vya wachezaji wake viendelee kuimarika bila kujihusisha na mambo mengine ambayo sio sahihi na kazi yao," alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza.

"Inaelezwa kuwa kocha havutiwi na viwango vya wachezaji kila wakitoka na kurudi majumbani kwao kwani siku wakikutana ni kama anaanza upya kuwaweka kwenye utimamu hali hiyo imemkwaza na kuwataka wachezaji warudi kutulia sehemu moja ili waweze kupambania taji la ligi na kombe la FA baada ya kushindwa kufikia malengo ya kucheza robo fainali."

Ndani ya misimu mitatu mfululizo ambayo Yanga imekuwa na mafanikio makubwa, ilikuwa na utaratibu wa kuweka kambi Avic.

Kambi hiyo imefanikisha Yanga kuchukua mataji tisa yakiwemo matatu ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA (3) na Ngao za Jamii (3).

Chini ya makocha wawili walioipa mafanikio Yanga kwa misimu mitatu mfululizo wakianza na Nabi, Yanga ilitwaa mataji mawili ya ligi, Ngao ya Jamii (2) na Kombe la FA kisha kuifanya timu hiyo icheze fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023.

Chini ya Miguel Gamondi ambaye ameondolewa kikosini Novemba 2024, pia aliendeleza utamaduni wa Nabi kwa kuiweka timu kambini msimu mmoja wa mafanikio kwake akitwaa taji la ligi na Kombe la FA huku akicheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2023-2024 ikiwa ni rekodi baada ya kupita takribani miaka 25.

"Baada ya mafanikio hayo, utaratibu ulibadilika ambapo msimu huu wachezaji walikuwa wakiingia kambini siku chache kabla ya mechi na sio kukaa muda mrefu kama zamani.

"Hali hiyo taratibu ikaifanya timu kushuka kiwango na mwisho wa siku tukapoteza mechi mbili mfululizo za ligi hali iliyofanya Kocha Gamondi aondolewe na kuja Ramovic," kilibainisha chanzo hicho.

Hata hivyo, Ramovic hajaanza vibaya sana ndani ya Yanga kwani ameiongoza timu hiyo kucheza mechi 11 za kimashindano akishinda saba, sare mbili na kupoteza mbili huku timu ikiishia makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.