Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaanza na ushindi Ligi Kuu ikipiga Pamba Jiji

Muktasari:

  • Yanga imecheza mechi tatu mfululizo za mashindano msimu huu bila kuruhusu bao huku ikifunga mabao saba.

Dar es Salaam. Yanga imeanza vyema Ligi Kuu msimu huu baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo, Jumatano, Septemba 24.09.2025.

Ushindi huo ni zaidi ya ule iliopata msimu uliopita ambapo katika mechi ya kwanza, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Katika mchezo wa leo, mashabiki wa Yanga waliokuwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa walionekana kutofurahishwa na namna timu hiyo ilivyocheza kipindi cha kwanza licha ya wenyeji hao kutoka na uongozi wa bao 1-0.

Licha ya kucheza vibaya mashabiki wakasubiri mpaka dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza kushangilia bao la kwanza mfungaji akiwa kiungo wao mpya Lassine Kouma kwa kichwa akimalizia kona ya Edmund John.

Bao hilo likaifanya Yanga kushusha presha ikimaliza dakika 45 za kwanza ikiwa inaongoza.

Kipindi cha pili Yanga ikabadilika ambapo mabadiliko ya wachezaji watano yakianzia dakika ya 56 yakairudishia ubora timu hiyo na kuanza kutengeneza mashambulizi makali.

Maxi Nzengeli akaipatia Yanga bao la pili dakika ya 61 akimalizia krosi ya beki wake wa kushoto Mohammed Hussein 'Tshabalala' akitoa pasi yake ya kwanza ya bao kwenye mchezo wa kwanza akianza kikosi cha kwanza cha Yanga.

Nzengeli kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi msimu uliopita alifunga bao la kwanza kipindi cha kwanza dhidi ya Kagera

Yanga ikaendelea kutawala mchezo na ikipata bao la tatu katika dakika za lala kwa kichwa cha Mudathir Yahya akimalizia krosi ya Pacome Zouzoua.

Hadi mwisho wa mchezo huo Yanga ikatoka na ushindi wa mabao 3-0,ikianza vyema mbio za ubingwa msimu huu.