Yanga kuanza na Bandari, Simba na Jamhuri Mapinduzi Cup

Dar es Salaam. Klabu ya Yanga itaanza kampeni zake za michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kucheza na Bandari ya Mombasa nchini Kenya Desemba 31 huku wapinzani wao wakubwa Simba ikifungua pazia lake, Januari Mosi 2024 kwa kucheza dhidi ya Jamhuri.
Yanga iliyopo kundi 'C' itacheza tena Januari 2 na KVZ kisha kuhitimisha hatua ya makundi kwa kucheza na Vital'O ya Burundi Januari 4.
Kwa upande wa Simba iliyopo kundi 'B' katika michuano hiyo itacheza na Singida Fountain Gate Januari 3, kisha kupambana na APR ya Rwanda Januari 5.
Ratiba kamili ya michuano hiyo itakayoanza Desemba 28 itazikutanisha mabingwa watetezi Mlandege watakaopambana dhidi ya URA ya Uganda huku Chipukizi United ikicheza na matajiri wa jiji la Dar es Salaam, Azam FC.
Michuano hiyo itaendelea tena Desemba 29 ambapo Vital'o itacheza na Bandari huku Jamhuri ikiikaribisha Singida Fountain Gate.
Desemba 30 itapigwa michezo miwili pia ambapo URA itacheza dhidi ya Chipukizi United huku Azam ikipambana na Mlandege wakati Desemba 31 itakuwa ni zamu ya Vital'o na KVZ.
Mchezo mwingine utakaopigwa Januari Mosi mbali na ule utakaozikutanisha Jamhuri na Simba, utakuwa kati ya Singida na APR huku Januari 2, URA itacheza na Azam FC.
Januari 3 kutakuwa na michezo miwili pia ambapo mbali na Simba kucheza na Singida ila APR itacheza na Jamhuri huku Januari 4 ikiwa ni zamu ya Mlandege itakayokuwa inacheza na Chipukizi United.
Michezo ya hatua ya makundi itahitimishwa Januari 5 ambapo mbali na mchezo wa Simba na APR ila KVZ itapambana dhidi ya Bandari.
Robo fainali itaanza kucheza kuanzia Januari 7 hadi 8 na nusu fainali ikichezwa Januari 10 huku fainali ikipigwa Januari 13.
Michezo hiyo yote itachezwa kwenye viwanja viwili pekee kuanzia mwanzo hadi mwisho ambavyo ni Amaan kil