Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool inavyokwenda kuchukua ubingwa wa 20 England

Muktasari:

  • Majogoo hao wa Anfield wamebakiza pointi moja kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu England.

Mashabiki wa Liverpool wanaweza kutembea kifua mbele kwa kile timu yao ilichokifanya mpaka sasa kwani Majogoo hao wa Anfield ni kama wameshamla ng’ombe mzima wakibakiza mkia kumaliza kazi.

Baada ya wapinzani wao wa karibu kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England, Arsenal kudodosha pointi mbili jana dhidi ya Crystal Palace kwa kupata sare ya mabao 2-2, ni dhahiri matokeo hayo yameifanya Liverpool ibakize pointi moja itwae taji hilo.

Liverpool imebakiza michezo mitano kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu England msimu huu huku mchezo unaofuata itakuwa kwenye uwanja wa nyumbani Jumapili, Aprili 27, kuikaribisha Tottenham.

Michezo mingine iliyosalia ni dhidi ya Chelsea, Arsenal, Brighton na Crystal Palace.

Huenda ikashuhudiwa Liverpool ikitangazia ubingwa kwenye uwanja wake wa nyumbani mbele ya mashabiki 61,276 lakini hilo litawezekana iwapo timu hiyo itapata matokeo chanya kati ya ushindi au sare.

Mechi dhidi ya Tottenham haitakuwa nyepesi lakini rekodi zinaonesha katika michezo 15 iliyopita ya mashindano yote waliyokutana kwenye uwanja wa Anfield, Liverpool imeshinda 11 na sare nne huku Tottenham ikiwa haijapata ushindi.

Iwapo Liverpool ikipoteza dhidi ya Tottenham, basi itasubiri mpaka Mei 3, mwaka huu itakapokuwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge kukabiliana na Chelsea kabla ya kuvaana na Arsenal Mei 10 kwenye uwanja wa Anfield.

Msimu wa 2019-2020, Liverpool ilitangaza ubingwa wa Ligi Kuu ikiwa imebakiza michezo saba mkononi tofauti na sasa ikiwa zimebaki mechi tano bado hawajafanya hivyo.

Msimu huo pia ilishuhudiwa Liverpool ikifikisha pointi 99 na kuwa timu ya pili England kukusanya idadi nyingi ya pointi ambapo vinara ni Manchester City wanaoshikilia rekodi ya kukusanya pointi 100 katika msimu wa 2017-2018.

Iwapo Liverpool itashinda taji la Ligi Kuu England msimu huu itafikisha jumla ya mataji 20 ya EPL kwenye makabati ya Anfield.