Wydad yaanza vibaya Kombe la Dunia ikilala kwa Man City

Muktasari:
Katika mchezo huo, Wydad ambayo anachezea kiungo wa zamani wa Yanga, Stephane Aziz Ki ilifungwa mabao hayo na nyota wa Man City, Phil Foden katika dakika ya pili na Jeremy Doku katika dakika ya 42.
Wydad Casablanca ya Morocco imeanza vibaya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu baada ya kuambulia kichapo cha mabao 2-0 kutoka Manchester City.
Katika mchezo huo, Wydad ambayo anachezea kiungo wa zamani wa Yanga, Stephane Aziz Ki ilifungwa mabao hayo na nyota wa Man City, Phil Foden katika dakika ya pili na Jeremy Doku katika dakika ya 42.

Pamoja na Wydad kujenga mashambulizi na kuingia hadi kwenye eneo la hatari la Manchester City, jitihada hizo hazikuzaa matunda hadi 90 zilipomalizika.
Mchezo huo umepigwa kwenye Uwanja wa Lincoln Financial jijini Philadelphia, Marekani na kushuhudiwa na mashabiki zaidi ya 60,000.
Kwa matokeo hayo Manchester City inaongoza kundi G ikiwa na pointi tatu.

Katika kundi hilo, mchezo unaofuata ni wa Al Ain kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) dhidi ya Juventus ya Italia utakaopigwa Saa 10:00 alfajiri ya Juni 19,2025.