Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wydad, Aziz KI mambo yamefika hapa

Casablanca, Morocco. Klabu ya Wydad Athletic ya Morocco hatimaye imekubali kumchukua kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki kwa mkataba wa kudumu, baada ya wiki kadhaa za sintofahamu kuhusu mustakabali wake ndani ya kikosi hicho.

Jana ilikuwa siku ya mwisho kwa klabu hiyo kudhibitisha kama itamchukua mchezaji huyo au la kutokana na mkataba wa miezi mitatu aliokuwa amesaini na klabu hiyo akitokea Yanga.

Aziz Ki, raia wa Burkina Faso mwenye umri wa miaka 29, alijiunga na Wydad Juni Mosi mwaka huu kwa mkataba wa muda mfupi, ili kuisaidia klabu hiyo katika michuano ya Kombe la Dunia la Klabu.

 Hata hivyo, baada ya kucheza dakika tisa pekee katika mashindano hayo ya FIFA, mashaka yalianza kuibuka iwapo Wydad wangesaini mkataba wa kudumu kabla ya tarehe ya mwisho ya Julai 10 ambayo iliyowekwa na klabu yake ya awali, Young Africans ya Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jarida la AfricaFoot, uongozi wa Wydad sasa umebadili msimamo na kuamua kumpa mchezaji huyo fursa ya pili.

Inaelezwa kuwa viongozi wa klabu wamefanikiwa kumshawishi kocha mkuu, Mohamed Amine Benhachem, ampe nafasi Aziz Ki kuonyesha uwezo wake katika msimu mpya wa ligi Kuu ya Morocco (Botola Pro).

Chanzo kingine cha uamuzi huo kinatajwa kuwa ni hatua ya Aziz Ki mwenyewe kukubali kupunguza kiwango cha mshahara alichokuwa akidai awali, jambo ambalo limewezesha klabu hiyo kufanikisha mpango wa kumbakiza rasmi.

Nyota huyo wa zamani wa ASEC Mimosas amekuwa akihusishwa na Wydad kwa muda mrefu, huku tetesi za uhamisho wake zikiripotiwa tangu mapema mwaka huu.

Sasa akiwa sehemu ya kikosi cha kihistoria cha Casablanca, Aziz Ki atakuwa na kiu ya kuonyesha kwa vitendo sababu iliyowafanya Wydad wamsajili rasmi.

Uamuzi huu unamaliza mvutano uliodumu kwa wiki kadhaa huku mashabiki wa Yanga wakiwa na maswali kuhusu hatma ya nyota huyo aliyewahi kuwa kiungo tegemeo wa klabu hiyo ya Tanzania.

Aziz Ki ni mmoja kati ya wachezaji mahiri kwa sasa akiwa alifanikiwa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu wa 2023/2023 ambapo alifunga mabao 21 huku mshindani wake Feisal Salum akifunga mabao 19.