Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uwanja wa Arusha kupewa jina la Rais Samia

Muktasari:

  • Akizungumza katika kipindi maalumu cha Wasafi Radio, jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema pendekezo hilo limebaki kwa Rais Samia kulipitisha.

Dar es Salaam. Uwanja mpya wa michezo utakaojengwa mkoani Arusha, unatarajiwa kupewa jina la Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika kipindi maalumu cha Wasafi Radio, jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema pendekezo hilo limebaki kwa Rais Samia kulipitisha.

“Tumependekeza hivyo kwa heshima ya mchango wa Rais Samia kwenye michezo, sanaa na utamaduni na Tanzania imefikia maendeleo makubwa,” amesema Msigwa.

Msigwa amesema uwanja huo unatarajia kuwa na uwezo wa kuingiza watazamaji 30,000 na utajengwa kwenye Kata ya Olmonti huko Arusha.

Eneo hilo kwa sasa linamilikiwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na lina ukubwa wa ekari 36.1.

Msigwa amesema ujenzi huo wa uwanja ni sehemu ya jitihada za Tanzania kuandaa fainali za Afcon 2027 na zitafanyika kwa ushirikiano na nchi za Kenya na Uganda.

“Kama Rais Samia Suluhu Hassan atapitisha pendekezo letu, uwanja utakapokamilika utabeba jina lake," amesema Msigwa.

Aidha, Msigwa amesema ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam utakamilika Agosti 24, mwaka huu.

"Viti vyote, jumla ya 60,000, vitabadilishwa na kuwekwa vipya. Ukarabati utakapokamilika, uwanja huo utakuwa umebadilika sana," amesema na kuongeza zaidi ya Sh31 bilioni zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa uwanja huo.

Mbali na Uwanja wa Benjamin Mkapa, uliopewa jina la Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Benjamin Mkapa, viwanja vingine vya michezo vyenye majina ya wakuu wa zamani wa wa nchi, ni Uwanja wa Kambarage, Shinyanga uliopewa jina la Rais wa Awamu ya Kwanza wa Tanzania, Hayati Julius Kambarage Nyerere na Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliopo Tabora, uliopewa jina la Rais wa Awamu ya pili, hayati Ali Hassan Mwinyi.