Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag: Man United haipo tayari kwa ligi

Muktasari:

  • United inafungua msimu mpya wa Ligi Kuu England Premier leo usiku wakati itakapokuwa kwenye Uwanja wa Old Trafford kuvaana na Fulham.

Manchester, England. Kocha wa Manchester United Erik ten Hag amesema timu yake haipo tayari kwa ajili ya Ligi Kuu England.

United inafungua msimu mpya wa Ligi Kuu England Premier leo usiku wakati itakapokuwa kwenye Uwanja wa Old Trafford kuvaana na Fulham.

Hata hivyo, wakati ikicheza leo kocha huyo mzoefu amewashtua mashabiki aliposema kuwa hawapo tayari hata kidogo kwa ajili ya ligi hiyo.

Amesema klabu hiyo iliharibu maandalizi yao ya msimu pre season jambo ambalo wanatakiwa kupambana nalo kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.

"Timu haipo tayari, lakini ligi inaanza, hatuwezi kujificha kwenye suala hilo lazima tupambane, lakini ni vyema kila mmoja akafahamu hilo."

Baadhi ya wachezaji wa United walichelewa kujiunga na kambi yao ya mazoezi nchini Marekani kutokana na kuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa.

Hivyo inaaminika kuwa hawataweza kucheza mchezo huu wa kwanza dhidi ya Fulham jambo ambalo limekuwa likimpa presha kubwa Ten Hag.

"Tulikuwa na baadhi ya wachezaji Marekani, lakini kumbuka kuwa wengine walikuwa na timu zao za Taifa kwenye Euro na Copa Amerika na baadhi wamesajiliwa hivi karibuni, bado wote hawana muunganiko wa timu.

Luke Shaw hatarajiwi kucheza kwenye mchezo huu kutokana na kusumbuliwa na majeraha huku kocha huyo akishindwa kuweka wazi kama atawatumia wachezaji wake wapya Martthijs de Ligt na Noussair Mazraoui waliojiunga na timu hiyo wakitokea Bayern.