Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag ajiweka levo za Ferguson, ataka makombe

Muktasari:

  • Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag, amesema lengo lake ni kushinda mataji msimu huu. Amekiri kuwa presha ni kubwa kutokana na matokeo ya timu msimu huu wa Ligi Kuu England.



Manchester, England. Kocha wa Manchester United, Erik ten Hag ameweka wazi kuwa lengo lake la kwanza pia msimu huu ni kushinda mataji na kusisitiza kwamba yeye ndio kocha bora wa timu hiyo tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson mwaka 2010.

Ten Hag, ambaye msimu uliopita aliilinda ajira yake baada ya kushinda taji la FA, amekuwa katika presha kubwa kutokana na kiwango ambacho timu yake imekionyesha tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu England.

“Mwaka huu tunataka kushinda mataji tena na ninajiamini. Kuna jambo moja tu muhimu katika soka ambalo ni kushinda taji mwisho wa msimu, nilipoingia kwenye timu nilitakiwa niijenge kikosi, tumenunua wachezaji vijana, na wengine tumewakuza na wametusaidia kushinda mataji

‘Ilinibidi nijenge klabu hii. Tulileta wachezaji wachanga ndani. Tuliendeleza wachezaji wachanga.Ninachojua, mashabiki wanafuraha na mimi, ingawa suala la kushinda mataji sio lengo langu mimi pekee ni lengo la Man United kwa ujumla,” alisema kocha huyo.

Kabla ya kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Liverpool jana, Man United ilishinda mechi moja na kufungwa moja huku ikishika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi.

Ten Hag alibakishwa katika kikosi cha Man United baada ya kikao na bosi wa timu hiyo Sir Jim Ratcliffe ambaye hapo awali aliripotiwa kufanya mazungumzo na Thomas Tuchel ili achukue mikoba ya Mholanzi huyo.

Katika misimu miwili aliyohudumu hadi sasa, Ten Hag alishinda taji la Carabao kwenye msimu wake wa kwanza kisha FA msimu uliopita, pia msimu wake wa kwanza alifika fainali ya mashindano hayo na kupoteza dhidi  ya majirani zao Manchester City.