Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sintofahamu kusimamishwa kipa Fountain Gate kisa Yanga

Muktasari:

  • Kipa John Noble alicheza dakika 45 za kipindi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Yanga na kuruhusu mabao mawili kati ya manne.

Dar es Salaam. Uongozi wa Fountain Gate unadaiwa kumsimamisha kipa wake Mnigeria, John Noble kwa makosa yanayodaiwa kuwa ni ya kizembe mna kuigharimu timu hiyo kukubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Yanga.

Noble amefungwa mabao mawili kati ya manne waliyofungwa na Yanga akicheza kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza kabla ya benchi la ufundi kufanya uamuzi wa kufanya mabadiliko kumwingiza kipa mwingine ambaye naye alifungwa mabao mawili.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo kimeliambia Mwananchi kuwa ni kweli wamefanya uamuzi wa kumsimamisha mchezaji huyo kutokana na kufanya makosa mawili yaliyoigharimu timu hiyo.

“Ni kweli tumemsimamisha hatujapendezwa na makosa aliyoyafanya ambayo yamesababisha timu yetu kuondolewa mchezoni kutokana na uzembe wa mtu mmoja ambaye ameighalimu timu nzima,” kimesema chanzo hicho.

Kocha wa Fountain Gate, Robert Matano baada ya mchezo wa jana dhidi ya Yanga alisema; “Golikipa leo amewapa mabao. Ametuangusha kabisa golikipa wa aina yake kufanya makosa kama yale, sasa kama tunacheza vizuri halafu tunapeana mabao vile itakuwa vigumu sisi kushinda,” alisema na kuongeza;

"Hawezi kufanya makosa kama yale golikipa wa kariba ya juu kama yeye ametutoa mchezoni kabisa, kwa mabao aliyofungwa hakuna timu yoyote hata Yanga pia wangeanza kufungwa mabao kama yale wangetoka mchezoni."

Alipotafutwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Issah Mbuzi kuthibitisha suala hilo alijibu kuwa hajui chochote na yeye anaona kwenye mitandao.

“Hata mimi naona kwenye mitandao tu, sijafahamishwa chochote na uongozi wangu wa juu, siwezi kuzungumza lolote juu ya suala hilo,” amesema Issa Mbuzi.

Fountain Gate imefungwa na Yanga jumla ya mabao 9-0 katika Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kufungwa 5-0 katika mechi yao ya mzunguko wa kwanza Desemba 29, 2024.