Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzize kinara ufungaji akipiga mbili na Fountain Gate

Muktasari:

  • Huu ni msimu wa kwanza kwa Clement Mzize kufunga zaidi ya mabao 10 kwenye msimu mmoja wa Ligi Kuu tangu alipoanza kuichezea Yanga.

Dar es Salaam. Clement Mzize amewapiku Prince Dube na Charles Ahoua wa Simba katika chati ya ufungaji bora kwenye Ligi Kuu baada ya leo Aprili, 21, 2025 kufunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Fountain Gate ambayo timu yake Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 4-9 kwenye Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa, Babati, Manyara.

Mabao hayo mawili ya Mzize katika mchezo huo umemfanya afikishe mabao 13, moja zaidi ya Dube na Ahoua ambao kabla ya mechi ya leo walikuwa wanaongoza, kila mmoja akipachika mabao 12.

Mzize ndiye alifungua karamu ya mabao kwa Yanga leo baada ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 38 alipotumia vyema makosa ya kipa John Noble wa Fountain Gate, kupangua vibaya mpira wa faulo wa Aziz Ki Stephane.

Dakika ya 43, Noble alifanya kosa lingine la kupiga pasi mkaa kwa Aziz Ki ambayo ilitumiwa vyema na nyota huyo wa Burkina Faso kuipatia Yanga bao la pili, matokeo ambayo yalibaki hivyo hadi filimbi ya mapumziko ilipopulizwa.

Yanga ilipata bao la tatu kupitia kwa Mzize tena katika dakika ya 70 baada ya mshambuliaji huyo kumalizia kwa shuti la mguu wa kulia pasi ya Jonathan Ikangalombo na bao la nne lilifungwa na Clatous Chama kwa mkwaju wa faulo uliokwenda moja kwa moja wavuni katika dakika ya 88.

Ushindi huo umeifanya Yanga ifikishe pointi 70 na hivyo kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu huku Fountain Gate ikibaki nafasi ya 11 ikiwa na pointi zake 29.

Mara baada ya mechi hiyo, Mzize alifanikiwa kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mechi.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, kocha wa Fountain Gate, Robert Matano amesema uzembe wa kipa wao John Noble umewagharimu.

"Magoli ya leo ni ya kupeana, Golikipa ametutoa kwenye mchezo, huwezi ukafanya makosa kama yale halafu utegemee timu kurudi mchezoni. Kwa makosa yale hata Yanga wenyewe wasingerudi mchezoni, Golikipa ametuangusha," amesema Matano.