Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida BS yaongeza machungu Simba, yaichomoa FA

Muktasari:

  • Yanga ilitinga fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuitoa JKT Tanzania huku Singida Black Stars ikifika hatua hiyo kwa kuitoa Simba.

Dar es Salaam. Singida Black Stars leo imetinga kibabe hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho  baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Simba leo kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara.

Matokeo hayo yanaifanya Simba ipoteze taji la pili msimu huu baada ya Jumapili iliyopita kulikosa taji la Kombe la Shirikisho Afrika mbele ya RS Berkane ya Morocco.

Ikitumia vyema makosa ya safu ya ulinzi ya Simba kwenye mchezo huo, Singida Black Stars ilipata mabao yake kupitia kwa Jonathan Sowah na Emmanuel Keyekeh.

Licha ya Simba kuanza mchezo ikionekana kuwa na hamu ya kutangulia kufunga bao la mapema, mambo yaliwabadilikia katika dakika ya 17 baada ya Sowah kufunga bao la kuongoza la Singida Black Stars.

Sowah alifunga bao hilo baada ya kumhadaa mlinzi wa Simba, Che Fondoh Malone na kupiga shuti la mguu wa kushoto lililojaa wavuni, akiitumia vyema pasi ya Arthur Bada.

Simba ilipata pigo katika dakika ya 28 baada ya kipa wake Moussa Camara kupata maumivu kutokana na mgongano wake na Sowah ambapo alilazimika kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Ally Salim.

Mabadiliko hayo yaliinufaisha Singida Black Stars kwani dakika sita baadaye, Keyekeh aliipatia bao la pili akitumia vyema kosa la Salim ambaye alipiga pasi iliyonaswa na kiungo huyo wa Singida ambaye hakufanya ajizi kuusukuma mpira huo wavuni.

Matokeo hayo yalidumu hadi mwamuzi Ahmed Arajiga alipopuliza filimbi ya kuashiria muda wa mapumziko.

Jahazi la Simba lilizamishwa rasmi katika dakika ya 48 na Keyekeh kupitia mkwaju wa faulo uliojaa moja moja wavuni ambao ulitokana na faulo aliyochezewa Edmund John nje kidogo ya eneo la hatari la Simba.

Baada ya kutangulia kwa mabao hayo matatu, Singida Black Stars ilionekana kurudisha idadi kubwa ya wachezaji nyuma ikionekana kuwa na mpango wa kuzuia na kushambulia kwa kushtukiza jambo lililoipa mwanya Simba kuwashambulia mara kwa mara.

Dakika ya 68, Jean Charles Ahoua aliipatia Simba bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa faulo uliojaa moja kwa moja wavuni, pigo ambalo walilipata baada ya Elie Mpanzu kufanyiwa faulo nje kidogo ya eneo la hatari la Singida Black Stars.

Licha ya Simba kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa wapinzani wao, safu ya ulinzi ya Singida Black Stars ilikuwa imara kulinda ushindi wao hadi filimbi ya mwisho ilipopulizwa.

Katika mchezo huo, Singida Black Stars ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Morice Chukwu, Jonathan Sowah, Edmund John, Mohamed Damaro na Frank Assinki ambao nafasi zao zilichukuliwa Anthony Tra Bi, Marouf Tchakei, Kelvin Nashoni, Victorien Adebayor na Elvis Rupia.

Simba mbali na badiliko la Camara kwa Salim, iliwatoa pia Valentine Nouma, Che Fondoh Malone, Yusuph Kagoma na Kibu Denis ambao nafasi zao zilichukuliwa na Mpanzu, Debora Fernandes, Mohamed Hussein na Chamou Karaboue.

Refa Arajiga kwenye mechi hiyo aliwaonyesha kadi za njano Damaro, Assinki na Chukwu wa Singida Black Stars huku kwa Simba akiwaonyesha Fabrice Ngoma na Karaboue kwa michezo isiyo ya kiungwana.

Kwa ushindi huo, Singida Black Stars itakutana na Yanga katika mechi ya fainali itakayochezwa kati ya Juni 26 hadi 28 mwaka huu