Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arajiga abebeshwa msalaba wa Simba, Singida BS

Mwamuzi Ahmed Arajiga

Muktasari:

  • Arajiga ni miongoni mwa marefa watatu wa Tanzania walioteuliwa kushiriki semina ya mwisho ya maandalizi kwa ajili ya Fainali za CHAN 2024 zitakazofanyika Kenya, Uganda na Tanzania, Agosti mwaka huu.

Dar es Salaam. Ahmed Arajiga ndiye mwamuzi atakayeshika filimbi katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho baina ya Simba na Singida Black Stars itakayochezwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati leo kuanzia saa 9:30 alasiri.

Huo ni mchezo wa pili kwa Arajiga kuichezesha Simba msimu huu, wa kwanza ukiwa ni wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu baina ya timu hiyo na Azam FC ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Lakini kwenye Kombe la Shirikisho, huo ni mchezo wa tatu wa nusu fainali kwa Arajiga kuchezesha ukihusisha Simba ambapo kabla ya hapo alichezesha nusu fainali za mwaka 2022 na 2021.

Katika nusu fainali ya 2021, Simba ilikutana na Azam FC katika Uwanja wa Majimaji, Songea na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Bao pekee la ushindi la Simba katika mchezo huo lilifungwa na winga Luis Miquissone na baadaye Simba ilitwaa ubingwa wa mashindano hayo.

Mchezo wa nusu fainali ya mwaka 2022, Simba ilikutana na Yanga katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ambapo ilipoteza kwa bao 1-0.

Shujaa wa Yanga katika mechi hiyo alikuwa ni kiungo Feisal Salum maarufu kama 'Fei Toto' na katika hatua ya fainali, Yanga ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo.

Katika mchezo wa leo, Arajiga atasaidiwa na waamuzi wasaidizi Glory Tesha na Athuman Rajab na refa wa akiba atakuwa ni Julius William.

Mchezo wa leo ni vita ya kihistoria inayobeba matumaini ya Singida Black Stars kuandika ukurasa mpya katika soka la Tanzania, huku kwa Simba ikiwa ni hatua ya lazima kufika fainali ili kupigania ubingwa huo baada ya kushindwa kulibakisha nyumbani Kombe la Shirikisho Afrika wikiendi iliyopita ilipolala kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Berkane.

Japo mechi hiyo inachezwa kwenye uwanja ambao hauna mwenyeji (neutral venue), kijiografia Babati ipo karibu zaidi na makazi ya Singida BS.

Mechi hii inakuja wakati Simba ikiwa na ratiba ngumu ndani ya siku saba itakuwa imecheza mechi yao ya tatu, ikitoka kuumana na RS Berkane ya Morocco katika fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika na kutoka sare ya bao 1-1 kisha Singida BS kwenye ligi.

Mshindi baina ya wababe hao atamenyama na Yanga ambayo tayari imeshatangulia fainali baada ya kuiondosha JKT Tanzania.