Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arajiga akabidhiwa rasmi Inonga, Mayele CAF

Muktasari:

  • Pyramids itakutana na FAR Rabat kwenye mchezo wa kwanza utakaopigwa Uwanja wa June 30 mjini Cairo, Misri, mechi ya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limemteua mwamuzi Ahmed Arajiga kuamua mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Pyramids ya Misri dhidi ya FAR Rabat ya Morocco.

Pyramids itakutana na FAR Rabat kwenye mchezo wa kwanza utakaopigwa Uwanja wa June 30 mjini Cairo, Misri, mechi ya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Ndani ya mchezo huo Arajiga atakuwa kwenye vita nyingine ya Simba na Yanga kutokana na kuwapo kwa Wakongomani wawili mshambuliaji Fiston Mayele anayeichezea Pyramids anayekutana na mshindani wake beki Henock Inonga.

Mayele alikuwa kwenye vita kubwa dhidi ya Inonga wakati wakiwa hapa Tanzania wakifanyiana bato ndani ya uwanja kuzipigania timu zao kipindi hicho Mayele akikipiga Yanga na Inonga akiwa Simba.

Arajiga atawakumbushia vita hiyo atakapokutana na wawili hao Aprili Mosi, 2025 kwenye mechi hiyo kabla ya timu hizo kwenda kumalizana wiki Moja baadaye nchini Morocco.

Mchezo huo sio tu utafuatiliwa zaidi na Waarabu, bali hata Watanzania mashabiki wa Simba na Yanga wakikumbushia juu ya wachezaji hao wawili ambao waliondoka hapa nchini kwa nyakati tofauti.