Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yala kiporo kwa ugumu ikiichapa Singida Black Stars

Muktasari:

  • Mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu baina ya Singida Black Stars

Dar es Salaam. Simba imekila vyema kiporo chake cha Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Black Stars baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi baina yao iliyochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Bao pekee la ushindi la Simba katika dakika ya 42 akimalizia kwa ustadi kwa mguu wa kulia pasi ya Jean Charles Ahoua.

Mukwala alitumia vyema makosa ya kipa wa Singida Black Stars, Obasogie Amas aliyeliacha mbali lango lake kujaribu kuuwahi mpira ambao Ahoua alimpasia mshambuliaji huyo, ambapo Mukwala alimzidi mjanja kwa kumpiga chenga kipa huyo na kuujaza mpira huo wavuni.

Hilo ni bao la 12 kwa Mukwala kwenye Ligi Kuu ambalo limemfanya amfikie Leonel Ateba ambaye anashika nafasi ya nne kwa kufumania nyavu nyuma ya kinara Jean Ahoua mwenye mabao 15 na Clement Mzize alite nafasi ya pili na Prince Dube wa tatu ambao kila mmoja amefunga mabao 13.

Kwa Ahoua, pasi hiyo ya mwisho aliyopiga imekuwa ya nane kwake kwenye Ligi Kuu msimu huu, jambo linalomfanya ashike nafasi ya tatu katika chati ya vinara wa kupiga pasi za mabao inayoongozwa na Feisal Salum mwenye 13 akifuatiwa na Maxi Nzengeli na Pacome Zouzoua ambao kila mmoja ana tisa huku Arthur Bada na Dube wakifuata kila mmoja akiwa na pasi za mwisho nane.

Baada ya kuingia bao hilo, Simba ilionekana kubadilika na kucheza kwa kujilinda zaidi huku Singida Black Stars wakishambulia katika muda mrefu wa mchezo lakini hadi filimbi ya mwisho ilipopulizwa na refa Hery Sasii wa Dar es Salaam, matokeo yalibaki hayo ya ushindi sa bao 1-0 kwa wenyeji.

Katika mechi hiyo, refa Sasii aliwaonyesha kadi za njano Kelvin Nashoni, Mohamed Damaro na Jonathan Sowah wa Singida Black Stars kwa kucheza rafu kama ilivyo kwa Chamou Karabou wa Simba huku pia kipa Moussa Camara wa wenyeji akipewa kadi ya njano kwa kosa la kupoteza muda.

Ushindi huo wa leo umeifanya Simba ifikishe pointi 72 na kubakia katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ambao unaongozwa na Yanga yeye pointi 73.

Singida Black Stats imebakia katika nafasi yake ya nne kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na ointi 53 ilizokusanya katika mechi 28.

Simba na Singida Black Stars zinatarajiwa kukutana tena keshokutwa Jumamosi katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB itakayochezwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.

Kwa kipa Moussa Camara kutoruhusu bao jana, amefikisha idadi ya michezo 17 aliyocheza bila nyavu zake kutikiswa (clean sheets) na hivyo anaongoza chati ya makipa waliofanya hivyo huku nyuma yake akiwepo Djigui Diarra wa Yanga ambaye amefanya hivyo katika mechi 15.

Kocha wa Simba, Fadlu Davids amesema kuwa timu yake haikuonyesha kiwango kizuri kwa sababu ya uchovu.

“Tumejitahidi kuiongoza mechi. Nyakati kama hizo ahuitajiki kucheza vizuri sana. Mechi iliyopita (ya Kombe la Shirikisho Afrika) wachezaji walikimbia sana hivyo tulipaswa kutunza nishati yetu, kuipooza mechi na kutocheza katika kasi ya juu na wachezaji wakaweza kufanya hivyo,” amesema Davids.

Kocha wa Singida Black Stars, David Ouma amesema kuwa timu yake imeonewa kwa kunyimwa penalti mbili.

“Timu bora imepoteza mechi. Kipindi cha pili timu yangu imeweza kuwazidi Simba. Kipindi cha kwanza kulikuwa na penalti na kipindi cha pili kulikuwa na penalti. Nahitaji penalti yangu. Najua baada ya maneno yangu nini kitatokea. Nawapa wachezaji wangu kongole kwa sababu ni ngumu kutathmini,” amesema Ouma.