Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simbu, Geay ngoma nzito Olimpiki, Tola akishinda kwa rekodi

Washindi wa mit

Muktasari:

  • Katika mbio za Marathon za Olimpiki zilizofanyika Ufaransa, Tamirati Tola wa Ethiopia alishinda na kuvunja rekodi ya zamani kwa muda wa saa 2:06:26, akipatia medali ya dhahabu.

Dar es Salaam. Wanariadha Alphonce Simbu na Gabriel Geay wameshindwa kufurukuta katika mbio za Marathon kilometa 42 kwa wanaume kwenye michezo ya Olimpiki inayoendelea huko Ufaransa huku Tamirati Tola akiibuka mshindi wa mbio hizo.

Tola (32) raia wa Ethiopia ameibuka mshindi akitumia muda wa saa 2:06:26 ambao ulimtosha kumfanya avunje rekodi ya kukimbia muda mfupi zaidi kwenye Olimpiki upande wa Marathon iliyowahi kuwekwa na Samuel Wanjiru Agosti 24, 2008 ya kukimbia kwa muda wa saa 2:06:32 wakati mashindano ya Olimpiki yalipofanyika Beijing, China.

Katika mbio za leo, Simbu alimaliza katika nafasi ya 17 akitumia muda wa saa 2:10:03 wakati Geay alishindwa kumaliza mbio.


Kilichotokea kwa Geay ni sawa na kilichomkuta gwiji wa Marathoni, Eliudi Kipchoge ambaye alishindwa pia kumaliza kwa kile kinachotajwa ni kutojisikia vizuri.

Kwa ushindi wa huo, Tola anakuwa Muethiopia wa nne kupata medali ya dhahabu katika Olimpiki kwenye mbio za Marathon akifuata nyayo za Abebe Bikila aliyeshinda mara mbili tofauti na Mamo Wolde.

Katika mbio hizo, Bashir Abdi wa Ubelgiji alishika nafasi ya pili akitumia muda wa saa 2:06:47 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Benson Kipruto wa Kenya aliyetumia muda wa saa 2:07:00.

Kenenisa Bekele ambaye alikuwa miongoni mwa wanariadha waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mbio hizo, alimaliza akiwa wa 39 baada ya kutumia muda wa saa 2:12:24.

Kwa kuibuka na ushindi wa medali ya dhahabu katika Marathon, Tola atapata kitita cha Dola 50,000 (Sh135 milioni) kutoka shirikisho la kimataifa la riadha (IAAF) ambalo liliahidi kutoa kiasi hicho cha fedha kwa kila mwanariadha atakayeshinda medali ya dhahabu katika Olimpiki mwaka huu.