Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yamvutia waya jezi namba sita wa Yanga

Muktasari:

  • Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe juzi katika mkutano na waandishi wa habari alisema wameshamaliza usajili na wataanza kutambulisha wachezaji na jezi namba sita atakuwa wa mwisho kutambulishwa

Wakati Yanga wakitamba Dar es Salaam kwamba kuna kitu jezi namba 6 kinatua kushtua nchi, imevuja kwamba hawajamalizana na mido jezi namba 6 wa Asec,  Mohamed Zougrana ambaye Simba wamemwekea mkataba mezani.

Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe juzi katika mkutano na waandishi wa habari alisema wameshamaliza usajili na wataanza kutambulisha wachezaji na jezi namba sita atakuwa wa mwisho kutambulishwa

"Kwa asilimia 100 usajili wa Yanga umeshafungwa wachezaji wote ambao tulikuwa tunawahitaji kwa ajili ya kwenda kuboresha benchi la ufundi kwa mujibu wa pendekezo la mwalimu wote tayari uongozi wameshamalizana nao kwa mikataba yao na wameshasaini"

" Tunasubiri zoezi la utambulisha jezi umalizike kama itakuwa katiki ya wiki kwahiyo  wiki hii haitafika mwisho tutaanza kushuisha vyuma, kuhusu jezi namba sita na mmeshindwa kumjua atakae vaa jezi namba sita Yanga msimu ujaio"

" Tayari usajili wetu umeshafungwa tunasubiri kuwatambulisha wachezaji"

Zougrana ambaye alionyesha uwezo wa juu kwenye michuano ya Caf msimu uliopita amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga ingawa mabosi wa timu hiyo bado hawajaweka wazi hatua za usajili huo lakini Wekundu hao wako naye mezani kuanzia wikiendi iliyopita wakipambana naye.

Zougrana ni kiungo aliyepiga kazi kubwa kwenye eneo la kati la ASEC wakiiishia nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na ubora wa kupiga pasi na hata kufunga.