Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaingia mitini mkutano kuelekea Kariakoo Derby, adhabu hii hapa

Muktasari:

  • Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 79 huku Simba ikishika nafasi ya pili na pointi 78.

Dar es Salaam. Simba imeshindwa kuhudhuria mkutano wa waandishi wa habari kwa ajili ya mchezo baina ya timu yao na Yanga kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 11:00 jioni.

Katika mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam leo, Kocha wa Simba, Fadlu Davids na mchezaji mmoja wa Simba walipaswa kushiriki lakini hawakutokea huku Yanga ikiwakilishwa na Kocha Mkuu Miloud Hamdi na nahodha msaidizi, Dickson Job.

Ofisa habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Karim Boimanda amesema kuwa wamefanya mawasiliano na Simba kufahamu kilichosababisha wasihudhurie mkutano huo.

“Tumewatafuta wenzetu wa Simba ili kufahamu nini ambacho kimewasibu na tumewakosa,” amesema Boimanda.

Kanuni ya 17(58) ya Ligi Kuu msimu huu inalazimisha timu kushiriki mkutano wa waandishi wa habari siku moja kabla ya mchezo.

“Kutakuwa na mkutano wa waandishi wa Habari siku moja kabla ya mchezo ambapo Kocha Mkuu na Nahodha au mchezaji mwenye Ushawishi ndani ya timu yake watazungumza katika mkutano huo,” inafafanua kanuni hiyo.

Kwa mujibu wa kanuni ya Ligi Kuu 40(5), kosa kama hilo linaweza kusababisha adhabu ya kifungo na faini inayofikia hadi Sh3 milioni.

“Kitendo chochote cha uvunjaji taratibu au ukiukaji mwingine wowote kanuni na taratibu kwa mujibu wa kanuni hizi ikiwemo taratibu za Usajili wa wachezaji au taratibu nyingine za undeshaji Ligi Kuu ambao haukuainishwa waziwazi kwenye kanuni hizi bado utastahili adhabu kwa muhusika kwa kupewa Onyo Kali au Karipio na/au faini kati ya shilingi laki tatu (300,000/-) mpaka shilingi milioni tatu (3,000,000/-) na/au kufungiwa kwa kipindi kati ya miezi mitatu (3) mpaka miezi ishirini na nne (24) au michezo kati ya mitatu (3) mpaka kumi (10),” inafafanua kanuni hiyo.