Semenyo mambo safi Man City
Muktasari:
- Arsenal, Charlton, Chelsea, Fulham, Millwall na Tottenham wote walikataa fursa ya kumsajili kabla ya hapo. Ndiyo maana nafasi aliyofikia sasa Semenyo mwenye umri wa miaka 25 ni ya kushangaza sana.
London, England. Habari ndo hiyo. Antoine Semenyo anatazamwa kama mchezaji ambaye anaweza kwenda kuamua mshindi wa Ligi Kuu England msimu huu.
Fowadi huyo wa kimataifa wa Ghana, Jumamosi alitazamiwa kucheza mechi yake ya mwisho kwenye kikosi cha Bournemouth wakati kilipomenyana na Arsenal, kabla ya kuelekea kwa wapinzani wao wa ubingwa, Manchester City, katika dili la Pauni 65 milioni.
Semenyo ndiye mchezaji anayewindwa zaidi England kwa sasa, lakini miaka kumi iliyopita alikuwa karibu kuacha kabisa soka. Akiwa na umri wa miaka 15, alikataliwa na Crystal Palace baada kufanya majaribio. Ilikuwa ni sehemu ya msururu wa kukataliwa uliomwacha Semenyo akilia na tayari kuamua kuachana na soka na kuzingatia kucheza mpira wa kikapu na marafiki zake.
Arsenal, Charlton, Chelsea, Fulham, Millwall na Tottenham wote walikataa fursa ya kumsajili kabla ya hapo. Ndiyo maana nafasi aliyofikia sasa Semenyo mwenye umri wa miaka 25 ni ya kushangaza sana.
Klabu kubwa zote za Ligi Kuu zimekuwa zikimfuatilia mshambuliaji huyo kutokana na kiwango chake bora akiwa Bournemouth. Semenyo huandika malengo yake ya msimu kwenye daftari mwanzoni mwa kila kampeni, na tayari yuko karibu kutimiza moja. Nyota huyo wa Ghana alilenga kufunga mabao kumi msimu huu na tayari ana mabao tisa baada ya mechi 19 tu.
Si ajabu klabu kubwa zote zilikuwa zikimtaka mshambuliaji huyo. Ana kipengele cha kuvunjwa kwa mkataba cha Pauni 65 milioni, ambacho lazima kitumike kabla ya muda wa wiki moja kuisha.
Bournemouth, bila shaka, wanataka nyota wao abaki hadi kufikia mwisho wa muda huo. The Cherries ina mechi mbili kubwa kabla ya hapo, wakianza kwa kuikaribisha Arsenal Jumamosi, kisha Tottenham Hotpurs, Jumatano ijayo. Semenyo atataka kuaga kwa mtindo wa kuvutia na Man City pia watakuwa na matumaini hayo.
Semenyo amekuwa akifanya mazoezi kivyake na kocha Saul Isaksson-Hurst, ambaye pia amekuwa akifanya kazi na wachezaji mahiri, akiwamo winga wa Arsenal, Noni Madueke.
Kocha huyo binafsi alisema: “Nilimwambia Antoine, ‘Wewe ni mchezaji wa Ligi ya Mabingwa. Unapaswa kucheza Ligi ya Mabingwa.’"